Bila shaka kichwa cha mada hii kinakuchanganya na unashindwa kuelewa nini nimedhamiria kukuambia, Lakini ambatana nami hadi mwisho mwa Makala hii utaelewa maeneo halisi ya mada hii ya leo. Karibu sana tujifunze pamoja ili tupate Maarifa ya kutusaidia. Wakati naendelea kusoma vitabu mbalimbali, nilikutana na jambo hili ambalo lilinishangaza kidogo, lakini nilijifunza mambo mengi sana muhimu katika safari ya mafanikio. Nimeyasoma na kujifunza kutoka kitabu cha K WANINI HADI WEWE SIO TAJIRI kilichoandikwa na Kocha Makirita Amani Nimeamua nikushirikishe maarifa haya nawe upate kujifunza , na kuchukua hatua ya kuyafanyia kazi. Mwandishi anaanza kwa kueleza yafuatayo; Huwezi kufikia utajiri mkubwa na mafanikio kwenye maisha bila ya KUTOA KAFARA. Mwandishi anaeleza dhana ya TRADE OFF akiwa na maana kwamba " Kupoteza kitu fulani ili kupata kitu kingine , au kuliwa eneo fulani ili uweze kula eneo jingine Kafara anayozungumzia mwandishi...
Hekima, Maarifa na Ufahamu Wekeza Saidia wengine