Skip to main content

KITABU CHA JUMA; My philosophy for successful living-Falsafa Yangu ya Maisha Ya Mafanikio Kilichoandikwa na Jim Rohn



KITABU CHA JUMA; My philosophy for successful living-Falsafa Yangu ya Maisha Ya Mafanikio  Kilichoandikwa na Jim Rohn.

Moja ya jambo muhimu sana katika dunia hii ya sasa ni kujifunza, ili kuweza kuwa bora zaidi katika jambo lolote huna budi kuwa na tabia ya kujifunza, 

Kupitia kujifunza tunapata maarifa ambayo yanaweza kutuvusha hatua moja kwenda hatua nyingine. Kufikia mafanikio makubwa sana katika maisha hatuna budi kujifunza kila siku

Watu wengi ambao wamefanikiwa wana tabia moja muhimu sana ambayo ni Kujifunza kila wakati na kila siku, shauku yao kubwa ni kujfunza na kujua mambo mengi ambayo yanawasaidia kukua zaidi 

Kupitia kujifunza, unapata nafasi ya kuyajua mambo mengi sana katika maisha.Hatuwezi kuyajua yote lakini tunatakiwa kujua mambo mengi.

Kama utapata nafasi ya kuwafutilia sana wale wanaojua mambo mengi katika Jamii , wana tabia ya kujifunza kila siku na kila wakati.

Hivyo, kama tunataka kufikia mafanikio makubwa na kufanya mambo kwa ubora hatuna budi ya kujifunza kila siku
Kama tunataka kuyajua mambo mengi katika dunia hii, hatuna budi  kujifunza kila siku.

Zipo njia mbalimbali ambazo tunaweza kuzitumia ili kujifunza, 

Lakini leo ninakushirikisha njia moja  ambayo  ni Kujifunza kupitia Kusoma Vitabu.
Maarifa mengi yamefichwa kwenye vitabu.
Waandishi wa vitabu wameyashirikisha maarifa waliyokuwa kwa kuandika vitabu.

Kupitia kusoma vitabu tunapata maarifa  mengi ya kujifunza, kufahamu  mambo mbalimbali kuhusiana na vitu ambavyo tunatamani kuvijua.

Hivyo, ni vyema sana kusoma vitabu hasa vinavyotoa maarifa sahihi kuhusiana na kile unachotaka kukifahamu.
Soma vitabu vile vinahusiana na kazi yako, biashara yako, na chochote kile unachohitaji kukifahamu.

Moja ya jambo ambalo ninalolifanya katika blogu hii ni kuhamasisha kusoma vitabu na kushirikisha yale ambayo tunajifunza kupitia kusoma.

Hivyo, basi kwa Juma hili tutakuwa na kitabu kizuri sana ambacho tutakwenda kujifunza,
Kinachoitwa My philosophy for Successful Living   Falsafa Yangu ya Maisha Ya Mafanikio  Kilichoandikwa na Jim Rohn.

Kitabu hiki kina mambo mengi sana ambayo kama tutayasoma na kuyachukua  tunakwenda kuwa na mafanikio makubwa sana.

Yaliyoandikwa humo ni maarifa aliyoyapata mwandishi katika safari ya kujifunza kuhusu maisha ya mafanikio.

Kitabu hiki kina kurasa 25 tu, kina Sura saba na ambazo ni fupi sana, najua hutashindwa kuzisoma.

Kwa juma hili lote, tutakuwa tukisoma kitabu hiki na kila mmoja aliyepata nafasi ya kukisoma ataruhusiwa kuchangia kile alichojifunza,

Na mwisho wa Juma hili utapata Makala Kamili Ya Uchambuzi wa Kitabu wa hiki..

Mambo machache ambayo tutakwenda kujifunza kutoka  katika kitabu hiki cha Juma ni haya yafuatayo;

    1.  Muda ni wa thamani sana kuliko fedha, unaweza kupata fedha za kutosha , lakini hauwezi  kupata muda wa kutosha.
Mwandishi anatupa ushauri wa kutumia muda wetu tulio nao kwa Hekima na kwa umakini mkubwa kwa sababu   muda ukishapita hauwezi kurudi tena.

  2. Elimu ya Darasani(Formal education) inakusaidia kupata ajira, lakini Elimu binafsi(self-education) ndiyo inayoweza kukufanya kuwa tajiri.

  3. Falsafa ya Kuzalisha zaidi na kufanya vizuri zaidi(Performance).
Siri kubwa ya mafanikio imefichwa katika kuwasaidia wengine.
Tafuta kila njia kuwatumikia/kuwasaidia wengine kufikia malengo yao.

  4. Fedha ni 'mchezo wa thamani'  Kadiri unavyotoa thamani , ndivyo unavyoweza kupata fedha zaidi.
Ili kupata fedha zaidi, tafuta zaidi kuongeza thamani katika kile unachokifanya.

  5. Ujue Msingi wa mafanikio yako na unatakiwa kuimarisha(fundamentals)
Kila kitu kina msingi wake(foundation), na msingi ukiwa Imara ndivyo unaweza kuendelea na kuimarika zaidi.

  6.  Chagua watu sahihi wa kushirikiana na wewe katika  safari ya mafanikio au katika jambo ambalo umekusudia kulifanya.
Hautafanya peke yako, unahitaji watu wa kuambatana na wewe , hivyo unatakiwa kuwa makini na katika kuchagua wale unaotaka kuambatana nao.

   7. Boresha na Imarisha falsafa yako binafsi ambayo umejitengenezea.
Katika maisha haya unapaswa kuwa na Falsafa yako ambayo itakuongoza katika maisha yako.Na unatakiwa kuiboresha na kuifanya imara kila wakati.

   8. Namna ya kufikia uhuru wa kifedha na kuondokana na madeni,
Kuwa na madeni ni utumwa, na yanaweza kukuzuia kutofika kule unakotaka kufika.

   ️9. Mambo sita muhimu ya kufanya ili uweze kuwa maisha bora(yasiyo ya kawaida-kiwango cha juu zaidi)
Extraordinary life.

Hayo ni mambo machache ambayo tutakwenda kujifunza kutoka katika kitabu hiki cha Juma

Hivyo nikukaribishe na nikuhamasishe uweze kukisoma kitabu hiki na  kufuatilia uchambuzi wake, najua tunakwenda kujifunza mambo mengi sana kutoka katika kitabu hiki.

Karibu sana tujumuike kwa pamoja kujifunza.
 Uchambuzi wa kitabu hiki kwa undani zaidi, utapata katika group la Whatsap la Elimu Ya Kitaa .

Kujiunga na group la whatsap la Elimu Kitaa tuma Sms Kwa njia ya  whatsap ikiwa na Jina Lako na Neno NIUNGE ELIMU KITAA  nawe utaunganishwa. Mfano; Joshua Golyama, NIUNGE ELIMU KITAA

Wako Joshua Golyama

Ahsante sana
_____________________________________________
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na;


Joshua Golyama, ambaye ni mwanafunzi Kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo(SUA-MOROGORO), Mhamasishaji wa Mafanikio na Mwandishi.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...