Je, umewahi kujiuliza kwanini watu wengi wanaanza biashara na baada ya muda mfupi wanaacha?
Na Kwanini biashara za watu fulani zinakuwa na wateja wengi kuliko biashara zingine
Nini siri ya Haya yote?
Karibu tujifunze kwa pamoja ili tupate majibu ya maswali yetu tunayojiuliza .
Jibu la swali letu kwa nini biashara nyingi zinakosa wateja na zingine kuwa na wateja wengi ni UBORA na THAMANI inayotolewa na Biashara husika.
Katika biashara yoyote ile yako mambo mawili makubwa ambayo wateja wanayaangalia.
1.Unafuu wa bei
2.Ubora wake.
Wateja wanataka kitu chenye bei rahisi na pia ambacho kina ubora.
Ukweli ni kwamba katika nyakati hizi za utandawazi hakuna baishara mpya au chochote kipya ambacho unaweza kukifanya.
Karibia kila kitu wapo watu wanakifanya.
Na hauwezi ukasema kwamba unaenda kufanya jambo jipya kabisa ambalo halijwahi kufanyika
Kila kitu/biashara wapo watu wanaoifanya baishara hiyo.Hivyo hauko peke yako unayeendesha biashara hiyo.
Ubora wako na thamani unayoitoa kwa wateja wako ndiyo itakayokufanya biashara yako kuendelea zaidi.
Mfano; wafanya baishara wawili wanaofanya baishara zinazofanana(bidhaa sawa), kitakachokwenda kuwatofautisha hapo in ule ubora wa bidhaa na thamani ambayo kila mmoja anayo litoa kwa wateja wa biashara hiyo.
Hata kama unafanya biashara inayofanana na mtu mwingine, tafuta kuwa tofauti naye kwa kuongeza thamani na ubora zaidi katika biashara yako.
Wanachokihitaji wateja ni Ubora na Thamani Kubwa ambayo unaitoa kwa wateja wako
Kama bidhaa zako hazina ubora, hakuna atakayekuja kununua.
Hii inajumuisha pia maisha ya kila siku na vile viti ambavyo tunavifanya kila siku
Lazima tuvifanye katika ubora wa hali ya juu sana.
Kinachotafutwa sasa ni ubora ulio nao .
Mhitimu anayetakiwa na anayetafutwa kuajiriwa si yule aliyefaulu pekee, bali mwenye elimu yenye ubora .
Kama elimu yake haina ubora hawezi kupata kazi.
Kila jambo linalofanyika linatakiwa kufanyika katika ubora.
Wanaohitimu vyuo vikuu na vyuo hapa nchini wako wengi sana, na kuna idadi kubwa sana ya wahitimu ambao wamesoma kitu kimoja na wote wanataka wakapate kazi.
Haitawekana kwa wote kupata kazi, ila kinachokwenda kuwatofautisha ni Ubora wa Elimu yao
Kampuni na taasisi mbalimbali zinahitaji kufanya na mtu aliye bora zaidi.
Najua hata wewe unapoenda sokoni/dukani kununua baadhi ya mahitaji ya nyumbani, unatafuta kilicho bora.
Kumbe , kwa ulimwengu wa sasa kinachotafutwa sana ni Ubora na Uthamani ulio nao.
Hata kama utakuwa na baishara nzuri na kubwa kiasi gani, kama haina ubora hiyo haifai na haiwezi kudumu kwa muda mrefu .
Hata viongozi wanaochaguliwa , wanatakiwa kuwa bora na ndivyo ambavyo watu wanataka watu wa aina hiyo.
Bila ya kuwa bora hauwezi kuwa kiongozi, bila ya kuwa bora baishara yako haiwezi kuendelea mbele zaidi.
Kwa maelezo hayo mafupi, nadhani umejifunza kitu kuhusiana na Ubora na umuhimu wake katika biashara na maisha ya kila siku.
Kwa kila jambo unalolipata kulifanya, lifanye katiak ubora.
Usifanye ili kumaliza, hapana bali fanya katika ubora .Ni heri ukatumia muda mwingi kulifanya jambo kwa ubora zaidi kuliko ukaliharakisha jambo na likose ubora .
Hata kama unafanya kazi ya mtu, labda umeajiriwa kufanya kazi katika kampuni fulani, mtumishi wa umma/serikalini na katika eneo lolote like hakikisha unalifanya katika ubora unaotakiwa.
Ukiwa bora katika jambo lolote unalolifanya , hakuna atakayekuzuia kutolipwa zaidi na kukua zaidi.
"If you become good at what you do, there is nothing that can stop you from getting paid more and promoted very faster"__Dan Kenedy
Ukiwa vizuri katika eneo lolote lile, hakuna atakayekuzuia kulipwa zaidi, hii ina maana kwamba katika biashara yako ukiwa bora na bidhaa zenye ubora hakuna atakayemzuia kuuza sana na kupata wateja wengi.
Kama unafanya biashara wekeza muda wako kutafuta buwa bora (excellence). Nguvu zako nyingi uzitumie kutafakari na kujua ni namna gani biashara yako inakwenda kuwa bora.
Uliyeajiriwa katika kampuni au unayefanya kazi serikalini , hakikisha unakuwa bora katika hicho unachokifanya.Muda wako mwingi utumie kufikiri ni namna gani utakuwa bora katika kazi yako.
Mwanafunzi shuleni, usisome tu ili uongoze darasani hapana, soma kwa bidii na huku ukitajua kuwa bora na sio kuwa wa kwanza.
Kama unataka kuwa mtu wa kwanza darasani hakikisha unakuwa wa kwanza katika ubora.
Elimu yako unayoitafuta hakikisha inakuwa na ubora.Elimu yako itakuwa na umuhimu na watu kukutafuta kufanya kazi na wewe pale utakapokuwa na elimu iliyo bora.
Namna gani ufanye ili kuwa bora!
Hadi hapa tulipofikia unaelewa na umetambua faida za kuwa bora katika kila unachokifanya.
Sasa ni namna gani unaweza kuwa bora
1.Fanya ubobezi katika jambo/kazi/biashara unayoifanya. Tafuta maarifa zaidi katika biashara yako/kazi yako unayoifanya.
Hakika unatafuta kujua kila kitu kinachohusiana na kazi au biashara yako ili uweze kuifanya katika ubora wa juu zaidi
2.Ambatana na wale ambao wako vizuri/waliofanikiwa zaidi kwenye kazi husika
Katika kila kazi/biashara inayofanyika wapo ambao tayari wamekuzidi kiwango fulani.Jifunze kutoka kwao namna gani wanaendesha/kufanya kazi zao na siri ya wao kufika hapo walipo.Hakikisha unajifunza katika kila hatua unayotaka kuifanya kutoka kwao na unakwenda kuwa bora zaidi.
3.Jifunze zaidi kuhusu kazi yako/biashara yako.
Kadiri ambavyo unakijua kitu vizuri ndivyo ubora wako unavyoongezeka.Hakikisha kila kitu kinachohusika katika baishara yako unakijua vyema. Tafuta kuboresha kila siku na kufikia kwenye ubora unaouhitaji.
4.Soma vitabu vinavyohusu fani /kazi yako
Kama ni biashara tafuta vitabu ambavyo vinafundisha kuhusu biashara visome na yale unayoyapata hakikisha unayatendea kazi.Kusoma tu kunakuwa hakuna maana kama hutayafanyia kazi maarifa unayoyapata.
Kulingana na kazi yako unayoifanya , tafuta na soma vitabu vinavyohusu kazi/huduma unayoitoa
5.Hudhuria semina, makongamano mbalimbali yahusuyo kazi yako
Yako makongamano mbalimbali , semina zinazofundisha namna ya kufanya jambo fulani.
Hakikisha unashiriki semina hizo na makongamano hayo ili uweze kuwa bora zaidi katika hicho unachokifanya.
Hatua Ya kuchukua;
Wekeza muda wako zaidi na nguvu zako kujua ni namna gani unaweza kuwa bora katika kazi yako/biashara yako.
Usifanye tu ili umalize, hapana fanya kwa ule ubora unaotakiwa.
Tafuta maarifa zaidi, jifunze zaidi, soma vitabu vingi kadiri uwezavyo, hudhuria semina/makongamano kuhusiana na kazi yako na yote unayoyapata yatendee kazi na utakuwa bora zaidi.
Natumai umejifunza kitu cha msingi sana leo, kichukue na hakikisha unakitendea kazi na unakwenda kuwa bora zaidi.
Chema chajiuza.
KARIBU KATIKA GROUP LA WHATSAP
Tuna group la whatsap letu la whatsap linaloitwa ELIMU KITAA , ambako huko tunapata nafasi ya kujadili mambo mbalimbali, Kurasa za Mafanikio, Hekima Ya Siku Uchambuzi wa Vitabu.
Karibu sana katika group hili tujifunze kwa pamoja.
Kujiunga tuma SMS kwa njia ya whatsap ikiambatana na jina lako na Neno NIUNGE
mfano; Joshua Golyama , NIUNGE kwenye namba hii 0764257495. Nawe utaunganishwa na group hili.
Ahsante sana
Joshua Golyama
Comments
Post a Comment