Skip to main content

KUTOA KAFARA ILI UWEZE KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA.



Bila shaka kichwa cha mada hii kinakuchanganya na unashindwa kuelewa nini nimedhamiria  kukuambia, Lakini ambatana nami hadi mwisho mwa Makala hii utaelewa maeneo halisi ya mada hii ya leo.

Karibu sana tujifunze pamoja ili tupate Maarifa ya kutusaidia.

Wakati naendelea kusoma vitabu mbalimbali, nilikutana na jambo hili ambalo lilinishangaza kidogo, lakini nilijifunza mambo mengi sana muhimu katika safari ya mafanikio.

Nimeyasoma na kujifunza kutoka kitabu cha KWANINI HADI WEWE SIO TAJIRI kilichoandikwa na Kocha Makirita Amani

Nimeamua nikushirikishe maarifa haya nawe upate kujifunza , na kuchukua hatua ya kuyafanyia kazi.

Mwandishi anaanza kwa kueleza yafuatayo; 
Huwezi kufikia utajiri mkubwa na mafanikio kwenye maisha bila ya KUTOA KAFARA.

Mwandishi anaeleza dhana ya TRADE OFF akiwa na maana kwamba " Kupoteza kitu fulani ili kupata kitu kingine , au kuliwa eneo fulani ili uweze kula eneo jingine 

Kafara anayozungumzia mwandishi siyo ya kuua watu kwa imani za kishirikina , bali ni kafara ya kukujengea nidhamu itakayokusaidia kufanikiwa sana.

Kafara ya kweli na itakayokusaidia na kukufanikisha kwenye mafanikio makubwa haimuhusishi mtu yeyote , bali inakuhusisha wewe mwenyewe, 

Tunazo rasilimali muhimu sana  ambazo ni nguvu na muda, 

Hapa ninakushirikisha namna ambavyo mwandishi anaeleza kuhusiana na kutoa kafara , 
Na kafara inayozungumza hapa ni ile inayokuhusu wewe , kuacha baadhi ya mambo fulani na kuyafanya mambo fulani ili kuweze kufanikiwa zaidi.

Maeneo matatu muhimu ambayo unapaswa kutoa kafara ili uweze kufanikiwa, 

 1; VITU UNAVYOFANYA

Kuna vitu vingi unapenda kufanya ambavyo havina mchango wowote kwenye mafanikio unayotaka katika maisha yako.
Hivyo vitu unapaswa kuacha kuvifanya mara moja.

 Je, ni namna gani unaweza kuacha?

Mwandishi anaeleza njia na namna sahihi ya kuacha kufanya.


Chukua karatasi na kalamu , Gawa pande mbili 

 Upande wa kwanza;

 Orodhesha vitu vyote ulivyofanya ndani ya wiki 1 , usiache hata kimoja andika vyote ambavyo umevifanya.
Hata kama umetembelea ndugu, umepiga stori na mambo mengine yote usiache hata kimoja.

 Upande wa pili; 

Orodhesha malengo unayoyafanyia kazi kwenye maisha yako, yaani kule unakotaka kufika.

Pitia upande wa 1 , jiulize kama kinakusaidia kufikia kipi kilichopo upande wa 2 yaani malengo yako.

Kama kina mchango weka alama hii ✅ 
Kama hakina mchango  weka  alama hii ❌ 

Yale uliyoyawekea alama ya ❌ usifanye tena katika maisha yako.
Fanya yale uliyoyawekea alama ya Vema tu(✅)

 2.MATUMIZI YAKO YA FEDHA

 Kanuni muhimu ni hizi zifuatazo kuhusiana na Fedha; 
 (1)Matumizi yako kuwa kidogo kuliko kipato na (2) Kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo ili izalishe zaidi.

Kuhusu matumizi yako ya fedha, mwandishi anatufundisha Yafuatayo (Fanya zoezi lifuatalo)


Orodhesha manunuzi yote ambayo umefanya ndani ya mwezi , Baada ya hapo,  pitia kila ulichonunua Je, ni kiti cha Muhimu kabisa kwenye maisha yako

Je,  maisha yasingeweza kwenda kama usingekuwa nacho? 
Kwenye kile ambacho maisha yangeweza kwenda bila ya kuwa nacho , kiwekee ❌ na usikinunue tena.

 3.WATU UNAOJIHUSISHA NAO

"Mafanikio yako ni wastani wa mafanikio ya watu watano unaotumia nao muda wako mwingi" 
Huwezi kamwe kuvuka nguvu ya watu watano wanaokuzunguka.

Fanya Yafuatayo kuhusiana na jambo hili;

✳️Orodhesha watu wote ambao huwa unatumia muda wako mwingi kuwa nao
Wale unaofanya nao kazi au biashata na wale wanaokuwa nao mara nyingi 

✳️Anza kupitia maisha ya kila mmoja , 
Angalia kiwango cha mafanikio ambacho wanacho, 
Angalia  malengo na mipango waliyo nayo je, ni watu wa kujituma kiasi gani , wenye kiu na mafanikio makubwa au la! 

✳️ Waondoe wote wale ambao hawana kiu ya mafanikio makubwa , wakatishao tamaa na walioridhika  na pale walipofika.
Hata kama unawapenda kiasi gani unatakiwa kuwaondoa.

Hayo ndiyo maeneo matatu muhimu ambayo unapaswa kutoa kafara ili kuweza kufanikiwa na kufika mbali zaidi 
Najua ni maumivu makubwa  sana utakayoyapata , lakini kwa kuwa umeamua kufanikiwa huna budi kutoa kafara.

 Mwisho;
Mafanikio yoyote yale ni mchakato na wala sio tukio na sio bahati, 
Ni lazima upambane, na ujitoe kikamilifu na yako mambo ambayo utatakiwa uyaacha hata kama ni mazuri kiasi gani, 

Kuna watu utatakiwa kuachana nao ili uweze kufanikiwa zaidi, hata kama umetoka nao mbali kiasi gani , kama hawana sifa unazozitaka huna budi kuachana nao.

Sio watu wote utaambatana nao, sio kila aina ya maisha utayaishi, na si kila fashion za nguo na za maisha zitakupitia , zingine lazima uziache ili ufike kule unatamani kufika.

Ahsante sana na Mungu akubariki sana.

 #Najifunza kutoka Elimu Kitaa Foundation.

See you Shining and enjoying the cake!; 

Wako 
Joshua E Golyama 
Simu; 0764 257 495
Email; golyamajoshua@gmail.com
Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...