Habari rafiki mpendwa ,
Karibu sana katika Makala hii Ya Kilimo na Ufugaji
Na leo tunakwenda kuangalia kuhusiana na Kilimo Cha Tembele.
Mboga nzuri sana na inayopenda na kutumiwa na watu wengi sana duniani
Makala hii itakuwa na Sehemu/Vipengele vifuatavyo;
1.Utangulizi
2.Aina za Tembele
3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele
4.Namna Ya Kuandaaa Shamba
5.Kupanda
6 Kuvuna
Karibu sana tujifunze kuhusu tembele.
Kilimo cha tembele
Kitaalamu tembele hujulikana kama ipomea batatas ni mboga ya nzuri ambayo asili yake ni amerika ya kusini, mboga hii ni nzuri sana na ni rahisi kulim a kwani;
• haiitaji nguvu nyingi kuihudumia zaidi ya kumwagilia maji na kuweka mbolea ya kutosha.
• Haina msimu, unaweza kulima msimu wowote, mradi maji yakiwepo.
Aina za tembele;
Kuna aina nyingi za tembele ambazo huwa na rangi mbalimbali, zifuatazo zinapatikana kwa wingi hapa Tanzania;
1. Tembele halisi yenye majani membamba
Hii ni aina ya tembele asilia mbayo huwa haizai viazi kwa chini ya udongo.
Picha inaonyesha tembele nyembamba
2. Tembele yenye majani mapana Hii ni aina ya tembele inayotokana na majani ya viazi vitamu, aina hii ina ladha nzuri sana ikiwa itaandaliwa na kupikwa vizuri.
Picha inaonyesha tembele pana
FAIDA ZA MBOGA YA TEMBELE KIAFYA ;
Tembele ni mboga yenye virutubisho muhimu vya mwili kama Vitamini C na Vitamini B kwa wingi na virutubisho vingine kama Vitamin A, K, B na madini muhimu kama Zinc, Iron, Calcium na protini.
Virutubisho hivi hufanya kazi zifuatazo mwilini;
i. Huzuia na kupunguza kansa
Tembele lina kiwango kidogo cha sukari yaani (low glucose content) hivyo hutumika kupunguza maradhi ya kisukari, mgonjwa anaweza kula tembele akiepusha mboga nyingine zenye sukari.
ii. Husaidia kuupa moyo afya nzuri
Tembele ina vitamini K ambayo husaidia kupunguza mabonge ya kalsium kwenye mishipa ya damu na pia hupunguza uvimbe wa mishipa ya damu na hivyo kupunguza magonjwa kama presha ya damu na mshtuko wa moyo.
iii. Inaongeza afya ya macho
iv. Hupunguza athari za bacteria mwilini.
v. Huimarisha afya ya mifupa.
vi. Husaidia damu kuganda kwa urahisi, sehemu yenye jeraha.
JINSI YA KUANDAA SHAMBA;
1. Tifua ardhi yako vizuri, vunja vunja vibonge vya udongo kutengeneza udongo laini
2. Changanya na mbolea kwa vipimo vifuatavyo;
Changanya ndoo moja kubwa ya mbolea ya kuku, mbuzi, ng’ombe, nguruwe n.k kwenye 1m2 (mita za square) kama udongo hauna rutuba ya kutosha baada ya kuchanganya vizuri udongo na mbolea
3. Tengeneza shamba lako vizuri kwa upana wa 1m na urefu uutakao, inulia tuta angalau 10cm pia weka kingo pembeni ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu wakati wa kumwagilia.
JINSI YA KUPANDA
1. Kata vipisi vya matembele vyenye urefu wa angalau 30cm
2. Panda kwenye ardhi huku macho ya kwenye matembele yakiangalia juu, kwa nafasi ya 15cm mstari kwa mstari na 15cm mche kwa mche .
3. Mwagilia vizuri.
UVUNAJI WA MBOGA HII
Uvunaji Mboga hii hufunga na kuzuia nyasi kuota, ikiwa tayari yaweza kuvunwa kwa kuchumwa.
Ahsante sana.
_______________________________________
Makala hii imeandaliwa na Kuandikwa na
Afisa Kilimo Wilfred Bernard Mawingo 0625708512
Kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo.
Anaendesha Mafunzo ya Mbogamboga Katika group la whatsap na pia anatoa ushauri na kuelekeza kuhusu kilimo cha Mbogamboga
Karibu sana ujiunge na Group hili la Mboga mboga uweze Kujifunza Kwa upana zaidi
Tuma sms kwa njia ya whatsap ili kujiunga na group kwa namba 0625708512.
Safi sana hii kitu sijawahi iona google
ReplyDelete