Habari rafiki mpendwa,
Karibu sana kama makala hii ya Kurasa za Mafanikio ili tujifunze na kupata mafanikio makubwa
Wakati tukiwa wadogo, wazazi walikuwa wanatukataza kucheza na kushirikiana na baadhi ya watoto/familia fulani, na endapo hutawasikiliza unapata adhabu kubwa sana.
Na walitukataza pia kutokula katika familia hizo.
Na zipo familia/watoto fulani ambao wazazi wanakuruhusu kwenda kucheza na kushirikiana nao na pengine wakakuruhusu kula chakula katika familia ile na hata kulala pale pale.
Na sababu kubwa ilikuwa ni kuhakikisha hatuharibiki katika tabia zetu .Na Katazo hilo lilikuwa linakuja baada ya Kutoridhishwa na tabia za watoto hao.
Jambo hili linaweza kutusaidia kujifunza machache kuhusu mchango wa wanaotuzunguka katika tabia zetu.
Ukiambatana na mwenye tabia ya wizi, bila shaka utajifunza kuhusu wizi .
Ukiambatana na mwenye tabia ya Uongo, bila shaka nawe utakuwa na tabia hiyo hiyo.
Ukiambatana na msengenyaji bila shaka yapo machache utajifunza kutoka kwake.
Tunaposoma Maandiko Matakatifu , tukajifunza kitu kizuri sana kuhusu wale wanotuzunguka.
Mithali 22:24 " Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi
Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi"
Usifanye urafiki na yule asiyependa kusoma kama wewe unataka kufaulu darasani usjie ukajifunza kuwa hivyo
Usifanye urafiki na muongo, kwa maana utajifunze tabia ya kuwa muongo
Usifanye urafiki na mtu asiyependa kuchukua hatua maana utajifunza kuwa na tabia hiyo.
Upo usemi unaosema "ukitembea na mwizi, nawe utakuwa mwizi"
Wale wanaokuzunguka wana mchangi mkubwa sana katika mafanikio yako, na mwenendo mzima wa maisha yako.
Kama unataka kufanikiwa katika maisha yako lazima uwe makini na aina ya watu unaombatana nao.
Ni lazima uchague watu walio sahihi kutokana na sehemu ile au mafanikio unayotaka kuyafikia katika maisha yako.
Aslimia 85 (85%) ya furaha yako na mafanikio inatokana na Aina ya mahusiano uliyo nayo.
Kadiri una vyokuwa na mahusiano mazuri na imara ndivyo unavyoweza kufanikiwa sana.
Na aina ya mauhsiano uliyo nayo yanatabiri ni mafanikio ya kiwango kipi na aina gani utakayokuwa nayo.
Vile unakuwa na mahusiano/urafiki chanya katika maisha yako, ndivyo nawe unavyokuwa chanya zaidi
Hii ina maana kuwa ukiambatana na watu waliofanikiwa/ wenye kiu na mafanikio nawe una nafasi kubwa sana ya kufanikiwa na kuwa kama wao.
Hii ina maana kuwa ukiambatana na watu waliofanikiwa/ wenye kiu na mafanikio nawe una nafasi kubwa sana ya kufanikiwa na kuwa kama wao.
Pia asilimia 90(90%) ya mafanikio yako , inategemea na wale wanakuzunguka(reference group)
Reference group(wanaokuzunguka) ni wale ambao unakuwa nao pamoja muda mwingi na baadhi ya vitu mnafanana katika kuvifanya.
Hivyo unatakiwa kuwa makini sana na wale wanaokuzunguka wakoje?
Sisi binadamu tunafananishwa na Kinyonga, ambaye hubadilika na kufanana na mazingira alipo kwa wakati ule.
Ndivyo ilivyo hata kwetu, tunachukua mitazamo, tabia, thamani na hata imani kutoka kwa wale wanaotuzunguka.
Hivyo unapochagua aina gani ya mtu unataka kuambatana naye, ni lazima ujifunze kwanza ana sifa zipi na je, zinazoweza kukusaidia wewe kufika sehemu sahihi /kule ulikokusudia.
Ambatana na wale walio na mitazamo chanya, wasiokata tamaa, wenye kiu na shauku ya kufanikiwa
Kama ni maanafunzi ambatana na wanafunzi wale wanaopenda kusoma , na usiambatane au kufanya urafiki na yule asiyependa kusoma, na asiye na kiu ya kufaulu mitihani
Kama unataka kuwa mtu aliyefanikiwa , huna budi kuambatana na wale wenye kiu na shauku ya kufanikiwa zaidi, na fanya urafiki nao.
Ambatana na wale mnaofanana vile unataka kufanya katika maisha yako.
Ondoka na uwe mbali sana na wale wenye mawazo hasi, mitazamo hasi na walalamikaji na wenye kulamumu kila wakati na sio watu wa kuchukua hatua.
" Kama unataka kuruka juu kama Tai, ambatana na tai utaweza kuruka.
Ukitaja kufanikiwa ambatana na waliofanikiwa au wenye shauku ya kufanikiwa. Kuwa makini sana na aina ya watu unaombatana nao kila siku, kwa sababu wana mchango mkubwa sana katika mafanikio yako.
_____________________________________
Makala hii imeandikwa na ;
Joshua Golyama, ambaye ni Mwalimu, Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo, Mhamasishaji Wa Mafanikio na Mwandishi.
+255 764 257 495 / +255 622 163 323
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com
Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com
Amen,, asante ujumbe mzuri sanaa,, shukran kwa kutukumbusha watu tupasao kushirikiana na kuambatana nao ili kufikia mafanikio yetu 🙏🙏🙏
ReplyDeleteAhsante sana, Ubarikiwe sana nawe kujifunza haya,
DeleteEndelea kutembelea tovuti hii kwa mafunzo mengi zaidi
Together brother ang
DeleteUbarikiwe sana, kaka karibu sana
Delete