FAHAMU KUHUSU PARACHICHI NA UMUHIMU WAKE MWILINI
Habari yako mpendwa,
Ni matumaini yangu kwamba u mzima na waendelea vyema na maisha ya kila siku, huku ukitafuta na kunia kufikia mafanikio makubwa sana maishani mwako.
Karibu sana tuweze kujifunza kuhusu Afya, na leo tunaangalia tunda linaloitwa parachichi pamoja na umuhimu katika mwili wa Mwanadamu.
Miongoni mwa vyakula vinavyohitajika ili kukamilisha mlo kamili ni MATUNDA, matunda hutupatia faida nyingi sana katika miili yetu .Yapo matunda mengi sana na yote yana faida kubwa sana katika Mwili wa Mwanadam.
Leo tunakwenda kufahamu kiundani kuhusu Parachichi na faida zake katika Mwili wa Mwanadamu.
Karibu sana ndugu yangu tujifunze na tuanze kulitumia tunda hili baada ya kujua faida nyingi tuzipatazo wakati tunatumia tunda hili
Parachichi (avocado) Persea americana
Habari yako mpendwa,
Ni matumaini yangu kwamba u mzima na waendelea vyema na maisha ya kila siku, huku ukitafuta na kunia kufikia mafanikio makubwa sana maishani mwako.
Karibu sana tuweze kujifunza kuhusu Afya, na leo tunaangalia tunda linaloitwa parachichi pamoja na umuhimu katika mwili wa Mwanadamu.
Miongoni mwa vyakula vinavyohitajika ili kukamilisha mlo kamili ni MATUNDA, matunda hutupatia faida nyingi sana katika miili yetu .Yapo matunda mengi sana na yote yana faida kubwa sana katika Mwili wa Mwanadam.
Leo tunakwenda kufahamu kiundani kuhusu Parachichi na faida zake katika Mwili wa Mwanadamu.
Karibu sana ndugu yangu tujifunze na tuanze kulitumia tunda hili baada ya kujua faida nyingi tuzipatazo wakati tunatumia tunda hili
Parachichi (avocado) Persea americana
Tunda aina ya parachichi hujulikana kama embefuta kwa sababu limejaa mafuta yenye faida nyingi sana katika afya ya mwanadamu
Tunda hili husifika sana kwa sababu lina virutubisho vyingi sana ambavyo vina umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu.
Chimbuko la Parachichi Kusini-Kati Mexico na America Ya Kati, miaka ya 7000 na 5000 B.C( Kabla Ya Kristo).
Parachichi ni tunda la kipekee sana .Vitabu vingi na tafiti nyingi zinaonyesha kuwa parachichi ni tunda lenye manufaa makubwa sana kiafya.
Virutubisho(nutrients) vinavyopatikana kwenye tunda aina ya parachichi.
Kutoka kipande kimoja cha parachichi(100 gram) kinatupa virutubisho hivi vifuatavyo;
Vitamini B-5 28% Copper 21%
Vtamini B-6 15% Folate 20%
Vitamini K 18% Vitamini B-6 15%
Vitamini B-2(Riboflavin) 10% Vitamini E 14%
Vitamini B-3(Niacin) 11% Potasium 10%
Magnesium 7% Manganese 6%
Vtamini B -1(Thiamine) 6% Zinc 6%
Chlorine 3% Vitamin D -
Vitamin B -12 -- Vitamini C 11%
Folate Husaidia seli za Mwili kufanya kazi vile inavyotakiwa (normal function) , na Asidi hii ya Folate muhimu sana kwa Mama mwenye mimba .
Lutein na Zeazonthin -Husaidia katika afya ya macho matatizo ya macho yanayotokana na umri.Husaidia na kuzuia jicho(macho) -seli na tishu za macho kutokuharibiwa na mwanga wa jua. Husafisha miale hatari ya mwanga na kuhakikisha selli za macho zinakuwa salama
Tafiti zinaonyesha pia kuwa endapo Karetonoid(Caretonoides) Yaani Luetin na Zeazonthin zikiwa za kutosha katika seli za jicho husaidia kuona vizuri.
Hizo ni baadhi ya virutubisho tunavyovipata kwa kula Parachichi. Lengo kubwa la Makal hii ni kukufahamisha kuhusu umuhimu wa parachichi katika afya yako. Baada ya kusoma makala hii, hakikisha unajitahidi kuongeza tunda hili la parachichi katika mlo wako ili usikose virutubisho vyingi sana na vya muhimu sana kwa afya yako.
FAIDA ZA KIAFYA ZITOKANAZO NA KULA PARACHICHI;
1.Parachichi ina virutubisho vitatu muhimu ambavyo miili yetu inategemea Wanga , Protein na Mafuta. Hivi virutubisho ni muhimu sana kwa afya ya binadamu kwani husaidia kuongeza nguvu za mwili , na kinga ya mwili pia.
2.Huboresha afya ya Ubongo(Healthy brain)
Katika parachichi tunapata madini ya Kopa(Copper) inayohusika na uzalishaji wa Myelin na kuhakikisha upatikanaji wake, husaidia katika Upokeaji na kutafsiriwa kwa taarifa kutoka vichocheo vya nje.
3.Hukuweka katika hali nzuri (mood ) nzuri.
Tafiti zinaonyesha kuwa watu wenye msongo wa mawazo wana upungufu mkubwa wa madini ya Kalsiam. Hivyo kutumia parachichi katika mlo wako kunaweza kusaidia kukuweka katika mood nzuri
4.Ni muhimu sana kwa Wamama wajawazito.
Kwa kuwa parachichi lina asidi ya Folate , Potasiam, Vitamini C na Vitaminj B-6 ambazo ni muhimu na husaidia afya na Ukuaji wa mtoto tumboni. Pia husaidia kupunguza hatari ya kuharibika kwa mimba changa.
5.Hupunguza hatari ya kupata magonjwa kama vile Unene uliopitiliza, Kisukari na magonjwa .
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kula mlo wenye mchanganyiko (mjumuisho ) wa matunda kama vile parachichi hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari na unene uliopitiliza(Obesity)
6.Parachichi ina mafuta mengi sana (fat ) lakini ni mafuta mazuri ambayo yanaitwa kwa Kiingereza "Mono unsaturated fats" ambayo ndiyo mafuta mafuta yanashauriwa kutumika katika chakula.
Aina hii ya mafuta husaidia katika afya ya moyo.
7.Parachichi husaidia umeng'enyaji wa chakula kufanyika vizuri(metabolic process).Mchakato wa kuvunja-vunja , virutubisho vilivyofonzwa na mwili ili kuweza kuzalisha nishati itakayotumika katika shughuli za mwili za kila siku.
8.Parachichi ina kiwango kikubwa sana cha Mafuta , ambayo ni "monounsaturated fats" ambayo ni mafuta mazuri-Husaidia kupunguza kiwango cha Cholestrol (lehemu )mwilini
Lehemu(cholestrol) ina madhara makubwa saba katika afya ya binadamu , kama itakuwa katika kiwango kikubwa. lakini pia cholestrol ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu kama itakuwa katika kiwango kinachotakiwa.
9.Parachichi inasaidia kusawazisha kiwango cha madini ya Sodiam kwenye miili yetu .Kuzidi kwa kiwango cha sodiam mwilini huongeza shinikizo la damu, pia huongeza hatari ya kufeli kwa moyo , kansa ya tumbo (stomach cancer) magonjwa ya figo na kiharusi .
10.Huzuia saratani .Hupunguza kasi ya ukuaji wa selu za saratani ya tezi dume.
Hadi hapo tumeweza kufahamu kwa uchache kuhusiana na Parachichi, virutubisho vinavyopatikana kwenye parachichi, na faida zake tuzipatazo.Kwa kuyajua haya tuna kila sababu ya kutumia tunda hili kwa wingi sana kutokana na umuhimu ambao tumeweza kuupata kupitia Makala hii
Ubarikiwe sana kwa Kujifunza hayaa.Yachukue na Anza kuyatendea kazi.
______________________________________________________________________________________________
Makala hii imeandikwa na ;
Joshua Golyama
Mwanafunzi wa Shahada Ya Awali Ya Sayansi Ya Kilimo
Chuo Kiikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA-MOROGORO)
+255764257495
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com
Blogu ; elimukitaa2020.blogspot.com


Comments
Post a Comment