KARIBU KATIKA MTANDAO WA ELIMU KITAA (STREET EDUCATION); Tujifunze kwa pamoja, ili tupate maarifa sahihi ya kutusaidia katika maisha yetu.
Rafiki yangu mpendwa;
Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na majukumu ya kila siku na unaendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuwa na maisha bora sana.
Moja ya kitu cha msingi sana katika maisha ambacho hutakiwi kukiacha ni kujifunza kila siku na kutafuta kuwa bora zaidi. Maisha ni sanaa, na kama ilivyo sanaa inahitaji ubunifu kila siku, usipotaka kujifunza kamwe hauwezi kuwa mbunifu. Hivyo, katika maisha hutakiwi kuacha kujifunza ili uweze kuwa bora zaidi.
Karibu sana katika Makala hii ambayo ni muhimu sana kwako na nimeifanya kuwa maalumu sana, kwa sababu nimekuandalia na kukuletea Makala hii ili uweze kujua hasa kwa undani kuhusu Mtandao huu wa Elimu KItaa (Street Education) chanzo chake, unahusika na nini, malengo yake na nini utakipata katika mtandao huu.
Karibu sana katika Makala hii uweze kuisoma ili uweze kujua hasa kwa undani kuhusu Mtandao huu wa Elimu Kitaa (Street Education) chanzo chake, unahusika na nini, malengo yake na nini utakipata katika mtandao huu.
Mtandao wa Elimu Kitaa (Street education) unahusika na kutoa maarifa mbalimbali kuhusu maisha, kujua kusudi la Mungu , vipawa vyetu.
Unahusika na kuchapisha Makala mtandaoni na mitandao ya kijamii, kuandika vitabu na kuwaleta watu wengi pamoja wenye shauku ya kufikia mafanikio zaidi katika maisha yao,Kujadili na kuchukua hatua.
MISINGI YA MTANDAO HUU WA ELIMU KITAA (STREET EDUCATION)
Kama unavyojua kila kitu/jambo linapoanzishwa linakuwa na misingi yake ambayo ndiyo mwongozo wa safari nzima ya mafanikio ya Jambo hilo. Kwa namna hiyo;
Mtandao huu wa Elimu Kitaa (Street Education) una msingi yake miwili ambayo inasimamia ambayo ni;
Mtandao huu wa Elimu Kitaa (Street Education) una misingi miwili ambayo ni;
- Hekima, Maarifa na Ufahamu
- Saidia wengine
Hekima, Maarifa na Ufahamu hutegemeana na yanafanya kazi pamoja, na humsaidia mtu namna ya kuishi na kujua kila jambo na namna gani anaweza kukabiliana nayo.
Mambo haya matatu ni ya msingi sana katika maisha ya Kila siku hii ni kutokana na umuhimu wake katika Nyanja zote za maisha ya Mwanadamu.
Ukweli ni kwamba pale mtu anapokuwa na mambo haya yote matatu anakuwa bora sana na kuweza kufanikiwa sana katika maisha yake.
Hekima, Maarifa na Ufahamu hutegemeana na yanafanya kazi pamoja, na humsaidia mtu namna ya kuishi na kujua kila jambo na namna gani anaweza kukabiliana nayo.
Ili tuweze kufikia mipango na malengo tuliyoipanga katika maisha yetu, haya matatu ni ya muhimu sana.
Unaposoma Maandiko Matakatifu tunakutana na jambo hili la Msingi sana.
Mithali 24:3-4
“Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na, kwa maarifa vyumba vyake hujazwa
Vitu vyote vya thamini na vya kupendeza”
Hekima, Maarifa na Ufahamu ni mambo ya msingi sana katika maisha ya Mwanadamu.
Lengo letu ni kuhakikisha kila mmoja wetu ana kuwa Ufahamu na Maarifa pia na kuweza kuyatumia maarifa aliyoyapata (Hekima). Karibu sana tuweze kwenda Pamoja.
Mtandao huu /programu hii umeanzisha kwa madhumuni ya kukusaidia wewe na watu wengi duniani kufikia ndoto zao kwa kutoa Maarifa sahihi ya namna gani tunaweza kufanikiwa katika kila nyanja za maisha yetu.
Ipo falsafa moja inayosema kuwa “ili wewe ufanikiwe ni lazima uwasaidie wengine kufikia mafanikio yao”
Maana hii kwamba pale unapohitaji jambo/kitu Fulani, saidia kwanza wengine kupata yale wanayoyahitaji.
Anza kwanza kufikiri ya wengine kwanza na kuwasaidia ndipo nawe uanze kufikiri ya kwako. Maandiko Matakatifu (Neno La Mungu) yanatutaka kufikiri ya wengine kwanza kabla ya kuyafikiri mambo yetu,na kuachana kabisa na ubinafsi na wivu wa kufanikiwa kwa wenzetu.
Fikiri kwanza kufanikisha wengine ndipo uanze kufikiri mambo ya kwako,Pale utakapowasaidia wengine kufikia mafanikio yao hakuna cha kukuzuia wewe kufanikiwa.
Tunawekeza zaidi katika kujua ni namna gani unaweza kufikia mafanikio yako, mojawapo kutoa maarifa sahihi kuhusu kulijua kusudi La Mungu na kujijua wewe ni nani na kile ambacho Mungu amekiumba kwa ajili ya wewe kukifanya hapa duniani.
MAKALA KATIKA MTANDAO HUU
Katika mtandao huuu wa Elimu kitaa utapata nafasi ya kuzisoma Makala ambazo zinawekwa kila siku. Mojawapo ya Makala utakazopata nafasi ya kuzisoma ni hizi zifuatazo;
1. MAKALA ZA KILIMO NA UFUGAJI
Unapata nafasi ya kujifunza kuhusu kilimo,kanuni za muhimu za kuzingatia katika shughuli za kilimo
Pia, utapata nafasi ya kujifunza kuhusu ufugaji na kanuni zake .
2. KURASA ZA MAFANIKIO
Ninakushirikisha maarifa na njia mbalimbali za mafanikio, unapata nafasi ya kufahamu kwa upana kuhusu mafanikio
Makala kuhusu ujasiriamali ,biashara na mambo mengine mengi yahusuyo biashara ,ujasiriamali na mafanikio kwa ujumla.
3. KUTOKA VITABUNI
Hapa unapata Makala zinazohusu maarifa, na mafundisho tunayoyapata kutoka kwenye Uchambuzi wa vitabu na kusoma vitabu. Unapata hamasa ya kusoma vitabu, faida zake na namna gani unaweza kusoma vitabu (tabia ya usomaji wa vitabu).
4. #NAJIFUNZA
Hapa ninakuletea yale ninayojifunza kila siku kwa kusoma vitabu Makala mbalimbali na chambuzi mbalimbali za vitabu na maisha kiujumla wake. Na wewe pia una nafasi ya kushiriksisha yale ambayo unajifunza kila siku
5. HEKIMA YA SIKU
Ninakushirikisha maarifa na njia mbalimbali za mafanikio, unapata nafasi ya kufahamu kwa upana kuhu mafanikio. Makala kuhusu ujasiriamali ,biashara na mambo mengine mengi yahusuyo biashara ,ujasiriamali na mafanikio kwa ujumla.
6. MAKALA YA JUMA
Hapa unapata Makala zinazohusu maarifa, na mafundisho tunayoyapata kutoka kwenye Uchambuzi wa vitabu na kusoma vitabu.
Unapata hamasa ya kusoma vitabu, faida zake na namna gani unaweza kusoma vitabu(tabia ya usomaji wa vitabu.
Ukweli ni kwamba, maarifa mengi sana yamefichwa vitabuni na kutokana na uvivu wetu tulionao wa kushindwa kusoma vitabu hivyo tunayakosa yale maarifa yaliyopo vitabuni
Hivyo nikukaribishe sana usikose kufutailia Makala hizi kila siku na kujifunza ili uweze kuwa bora zaidi katika maisha yako na kufikia mafanikio makubwa
Hizo ndizo Makala ambazo utazisoma katika mtandao huu wa Elimu Kitaa (Street education). Lengo kubwa ni kuhakikisha kila mmoja wetu anapata maarifa sahihi yatakayomwezesha kufikia mafanikio makubwa katika maisha yetu.
Hekima,Maarifa na Ufahamu ni mambo ya msingi sana katika maisha ya Mwanadamu Tunachokitafuta hapa ni kuwa na hayo yote matatu katika maisha yetu, Tunaweza kupata maarifa sahihi kwa Kumcha Bwana.
Mithali 1:7 “Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa”
Tunaweza pia kupata maarifa kwa Kusoma Vitabu vyenye mafundisho sahihi na Kujifunza pia kupitia wengine kwa kusoma Makala kama hizi, na mitandao ya Kijamii.
NAMNA YA KUSHIRIKI KATIKA MTANDAO HUU
Mtandao huu wa Elimu Kitaa (Street Education) unatambua mchango wako, na hakuna ambaye anayajua mambo yote, Hivyo basi tunakupa nafasi ya wewe kushiriki nasi katika nasi katika kuijfunza kwa kutuandikia maoni yako mwishoni mwa makala hii ambayo umeisoma.
Au unaweza kuwasiliana na kututumia maoni yako kwa kutuandikia hapo chini kabisa kwenye tovuti hii na maoni yako tutayapokea. Pia, unaweza kutuandikia kwa njia ya Baruapepe (Email: golyamajoshua@gmail.com.
KARIBU KATIKA MTANDAO WA ELIMU KITAA (STREET EDUCATION)
Lengo la makala ya siku ya leo nikukukaribisha ndugu yangu katika mtandao huu wa Elimu Kitaa ili tuweze kujifunza na kupata maarifa sahihi katika maisha yetu na kuwa bora zaidi.
Tunatafuta kuwa na Hekima, Maarifa na Ufahamu ili tuweze kuwa na maisha bora kabisa na kufikia kule tunakotakiwa.
Zifuatazo ni njiia ambazo unaweza kuzitumia kujiunga nasi.
1. Kwa kujiunga na mfumo wetu wa E-mail, kwa kujaza Fomu yenye taarifa muhimu kama jina lako, na Email yako. Kwa kujiunga na mfumo huu wa E-mail utakuwa ukipokea kila siku kupitia email yako.
2.Kujiunga na group letu la facebook linaloitwa ELIMU KITAA (STREET EDUCATION).
Katika kundi hili la facebook kutakuwa na mijadala mbalimbali na maswali kuhusu maisha na namna gani tunaweza kufanya ili kuweza kufanikiwa katika maeneo tunayotamani kufika. Kama unahitaji kujiunga na group hili la facebook, unawezalitafuta mtandaoni na ukaweza kujiunga.
3.Like na fuatilia ukurasa wetu wa facebok wa Elimu kitaa.
Ukurasa huu wa Elimu Kitaa unakushirikisha makala mbalimbali ambazo zinakuwa zinarushwa kwenye tovuti ya Elimu Kitaa.
4.Jiunge na channel yetu ya Elimu Kitaa Foundation na group letu la Elimu Kitaa inayopatikana katika mtandao wa Telegram.
Huku pia utapata Makala na majadiliano mbalimbali yatajadiliwa huku na Pia utapata uchambuzi wa Kitabu na kupata nakala ya kitabu hicho.
Elimu Kitaa Foundation: t.me/elimukitaa Elimu Kitaa (Street Education): https://t.me/joinchat/LHzGxk_tLQu8Mv-hoBoXcQ
5.Unaweza kujiunga na Group la wasap la Elimu Kitaa ili kuendelea kujifunza zaidi na kupata maarifa sahihi kuhusu maisha. Makala za Hekima Ya Siku, Kurasa za Mafanikio na Chambuzi za Vitabu utazipata huko katika group la wasap.
Kama unahitaji kujiunga na group hili la wasap tuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye maneno haya; Jina lako ikifuatiwa na maneno haya NIUNGE ELIMU KITAA Mfano, Joshua Golyama NIUNGE ELIMU KITAA nawe utaweza kuunganishwa.
Tuma sms kwa njia ya whatsap kwa namba hii 0764257495.
Ni matumaini yangu kwamba umenielewa vizuri sana na kujua vizuri sana kuhusu kile ambacho kinachoendelea katika mtandao wetu wa Elimu Kitaa (Street Education).
Hivyo, nachukua nafasi hii kukukaribisha kwa moyo mmoja kushirikiana nami katika mtandao huu na pia kujiunga na kutembelea kuzisoma Makala zote ambazo zinakuwa zinawekwa kila siku na zenye maarifa ya Kutosha ya kukusaidia kuweza kufika mbali zaidi katika maisha yetu.
Mungu akubariki sana kwa kusoma Makala hii, na ahsante sana kwa muda wako uliotumia kuisoma.
Kwa maoni na Ushauri wasiliana nami
Simu: +255 764 257 495/ +255 622 163 323
Email: golyamajoshua@gmail.com
Blogu: elimukitaa2020.blogspot.com
Wako Joshua Golyama
Ahsante sana
_____________________________________________
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na;
Joshua Golyama, ambaye ni mwanafunzi Kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo(SUA-MOROGORO), Mhamasishaji wa Mafanikio na Mwandishi.


Comments
Post a Comment