Skip to main content

KURASA 05; KUJITAMBUA, Na umuhimu wake katika maisha ya kila siku


" Kujitambua"  maana  yake  nini??
Unaelewa  nini  kuhusiana  na  neno Hili Kujitambua?.
' Kujitambua '  limetokana  na  neno Tambua lenye maana ya kujua/kuelewa

Hivyo; Kujitambua ni hali ya mtu binafsi kujielewa vile alivyo. Au uwezo wa mtu binafsi kung'amua yeye ni nani?, Anapaswa kufanya nini na kwa sababu ipi na lini?
Pia, Kujitambua ni uwezo wa mtu  binafsi  kujielewa vizuri kuhusu yeye, tabia zake , majibu yake na vyote vile ambavyo vinamzunguka.

 Katika suala hili ya kujitambua , mtu huyu lazima aweze kuyaelewa mambo yafuatayo kuhusu yeye ; 

Yeye ni nani? (Mimi ni nani?)

Uwezo wake (wako binafsi) ni upi? 
Hapa naamanisha (upekee wako ulionao ) kunakopelekea utofauti wako na watu wengine

Nini  natakiwa kukifanya hapa duniani?

Unaelekea wapi ?

Mchango wako  kwa jamii inayokuzunguka ni upi??

👆 hayo ni mambo ambayo mtu anayejitambua anatakiwa kuyaelewa na kuyafahamu vizuri kabisa

Kujitambua(Self-awareness) ni jambo la muhimu sana kila mtu kulifahamu

Ni muhimu sana kila mmoja kujitambua vile alivyo ili aweze kujua namna sahihi ya kuishi

 Usipojitambua wewe binafsi, utapata taabu sana na hutaweza kujua ni namna gani uishi,


Jijue wewe hasa ni nani? Uwezo wako binafsi,  madhaifu yako(changamoto)

Namna unavyopokea taarifa nzuri/mbaya, Pale mtu anapokukosea , unalipokeaje?  mazungumzo yako yakoje?
Na kuelewa namna unavyodhibiti hisia zako

Ni mambo ya msingi sana kuyajua

Maswali Matano Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Na Kuweza Kupata Majibu Yake.

- ili uweze kujitambua wewe ni nani hasa,  na kujielewa vizuri.Haya maswali matano ni miongoni mwa maswali muhimu sana ambayo unapaswa kujiuliza ili uweze kujijua na kujielewa vizuri wewe binafsi

1.Mimi ni nani?

2.Kitu gani naweza kukifanya katika ubora zaidi kuliko kitu kingine chochote?

3.Kwanini niko hapa?

4.Ninafanya nini hapa na kwanini?

5.Ninaelekea wapi??

 Maswali haya si marahisi sana yanakutaka kukaa chini na kupata utulivu wa hali ya juu sana ili uweze kupata majibu yake.

Vile unavyopata majibu sahihi juu ya maswali haya ndivyo unavyoweza kujitambua na kujijua vizuri kuhusu wewe!😀

MATOKEO YA KUJITAMBUA
Haya ni matokeo ya mtu kujitambua;
🖊️ Anakuwa na *Nidhamu* (self-discipline)
🖊️Kuleta Kujiamini (self-confidence)
🖊️ Msimamo
🖊️Ujasiri
🖊️Na Mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka

Mtu anayejitambua ni mtu ambaye anakuwa na maamuzi mazuri na kabla ya kufanya jambo hufikiria zaidi na kuja na maamuzi mazuri yenye manufaa juu ya jambo fulani

Kujitambua inatusaidia kuwa bora katika kila jambo tunalolifanya,
Mfano; kazini kwake, shuleni na mahali popote anapokuwa na lolote alifanyalo hulifanya katika ubora zaidi

Unapokuwa unajitambua na kujijua vizuri kunakusaidia kuishi maisha yako halisi, yale maisha ambayo unatakiwa kuyaishi
Na hakuna ambaye atakuyumbisha
Na pengine kutohangaika na namna dunia inavyokwenda.

Ukijitambua unakuwa makini na hisia zako na namna gani unavyoweza kudhibiti
Mfano,  Hasira
Vile tunavyoyapokea  mambo mbalimbali tunayokutana nayo kila siku.

Na majibu yetu pale jambo lolote linapotokea katika maisha yetu.

 Pia kujitambua kunaimarisha mahusiano yetu na wale wanaotuzunguka. Kwa sababu unajijua vizuri wewe ulivyo , wapi uko vizuri na wapo ambapo hauko vizuri.

📌  Anayejitambua anakuwa makini na vile vitu anavyovifanya na kamwe hawezi kupoteza muda kabisa
Atauthamini sana muda wake  alio nao.

📌 Huwezi kuona yule anayejitambua vizuru analalamika-lalamika 😀😃
Kwa jambo lolote linalotokea katika mazingira yanayomzunguka

"Mazingira yanayomzunguka hayawezi kumsumbua kabisa".

Nini Kinaweza Kutokea Kama Mtu Hatajitambua?
Mazingira yatamsumbua sana(mtumwa wa mazingira) Na mahusiano yake na watu wanaomzunguka hayatakuwa mazuru kabisa(hatojali wengine).

Usipilojitambua na kujijua wewe ni nani hautaweza kuishi maisha yako halisi 
Utaishi kwa kufuata wengine wanafanya nini na sio kile wewe unahitaji kukifanya.

Usipojitambua wewe mwenyewe utahangaika sana kufanya kila kitu hapa duniani
Si kila jambo linalofanyika hapa duniani unatakiwa kulifanya.

Usipojitambua wewe mwenyewe hauwezi kujua hatima ya maisha yako.

 Umeumbwa kwa kusudi maalumu

Haujaumbwa kwa bahati mbaya na hukuja duniani kama ajali

Hapana umekuja duniani kulitimiza lile Mungu amekuumba kulifanya na kulitimiza .

Unapojitambua wewe mwenyewe unakuwa na nidhamu binafsi

Na utatumia na kuuthamini muda wako vizuri sana.
Hautakubali kupoteza muda wako na kutumia nguvu  zako nyingi kwenye mambo yasiyo na maana.

Kujitambua wewe mwenyewe , unapata kujiamini zaidi , na kupata nguvu na kufurahia kile ambacho unakifanya.

Ili kujijua na kujua hatima ya maisha yako ni lazima
Utafute majibu ya Swali hili " MIMI NI NANI?

Tunachokitafuta hapa ni kuishi maisha yetu halisi , maisha yale Mungu amepanga kwa ajili yetu.

Mimi  ni nani?
Jibu la swali hili litakusaidia kujikita katika jambo moja tu, lile limekuleta wewe hapa duniani (Kusudi La Mungu Katika maisha yako).

Jibu la swali hili litakusaidia na kukuwezesha kutogharikishwa na mazingira ya nje na vyote unavyokutana navyo hapo katikati
Havitaweza kukuzuia na kukusumbua kwa sababu unajijua vizuri wewe binafsi

Fasheni mpya za kila siku,  na   maisha ya watu wengine namna wanavyoyaendesha
Havitakusumbua kwa kuwa unafahamu nini unatakiwa  kukifanya chini ya jua

Mwisho; Tambua wewe ni nani? Kijue kile ambacho unapaswa kukifanya .
Jikite zaidi kufanya kitu hicho na kukiishi utaweza kufanikiwa sana, na kufikia pale Mungu amekusudia uweze kufika.

Kujiunga na Group la whtasap ; Tuma SMS yenye  Jina lako pamoja  na Neno NIUNGE ELIMU KITAA  kwenda Namba 0764 257 495.(Mfano Joshua Golyama NIUNGE ELIMU KITAA
Karibu sana.

Wako Joshua Golyama.

Simu; 0764 257 495/0622 163 323.

Email; elimukitaa2020@gmail.com /golyamajoshua@gmail.com

Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com.



Comments