Skip to main content

Posts

Showing posts with the label KURASA ZA MAFANIKIO

ANZA SASA, UMRI USIWE KIKWAZO CHA WEWE KUTOTIMIZA NDOTO ZAKO

 ANZA SASA KUFANYA, UMRI ISIWE KIKWAZO KWAKO. Bila shaka unayo maono fulani (Unajiona ukiwa unafanya kitu baadaye ambacho ni kikubwa sana). Kwa namna fulani unatambua jambo fulani unaweza kulifanya kwa ufanisi mkubwa kabisa. Na unajua kabisa, kwamba utakapofanya jambo lile utakuwa katika viwango fulani vikubwa sana. Lakini, mbona huanzi? Nini kinakukwamisha usiendelee?  Ni ujuzi, Maarifa, huelewi pa kuanzia? Au unasema ngoja nikue kidogo au nifikie hatua fulani?. Tuko watu ambao tunasubiri hadi tufike viwango fulani vya Elimu ndipo tuanze kutumiza ndoto zetu. Tuko watu tunaosubiri tufikie Umri fulani ili tuanze kutimiza ndoto zetu. Lakini tunajichelewesha wenyewe, umri sio tatizo kabisa. Kwani haujaona Watu wakiwa na Umri mdogo na wanafanya Makubwa?. Je, Mastaa wengi katika tasnina mbalimbali duniani wana Miaka mingapi hadi muda huu na walianza wakiwa na Miaka mingapi? Je, Mabilionea wa Dunia wana Miaka mingapi muda huu?. Je unamfahamu Rev Victor Githu  kutoka Kenya ...

JENGA TABIA YA KUJIFUNZA KILA WAKATI , ONDOA KIBURI KATIKA KUJIFUNZA.

JENGA TABIA YA KUJIFUNZA KILA WAKATI ,  ONDOA KIBURI KATIKA KUJIFUNZA. Unapokosa tabia ya kujifunza na kuwa na hali ya kujiona unajua kila kitu utakuwa nayo na Kwa Maana Hiyo hautaweza kuwa na spirit ya kuendelea kujifunza zaidi na zaidi. Lakini unapokuwa unajifunza kila wakati, utagundua kwamba Mambo mengi huyajui hii itaamusha Nguvu mpya, ari mpya na hamasa ya kue ndelea kujifunza zaidi. Jifunze zaidi ili upate hamasa ya kujifunza zaidi. Na MUHIMU,  ili uweze kujifunza ni lazima ujione hujui , na kama utaona kama unajua kamwe hautaweza kujifunza Kwa maneno Mengine unakuwa na KIBURI KATIKA KUJIFUNZA ambacho Kinakuzuia wewe kujifunza zaidi, kwa sababu ndani yako kutakuwa na Sauti kama hii  'mbona kila kitu ninakijua, kujifunza ni kupoteza muda' Hakikisha unajitahidi unakuwa na Tabia Ya KUJIFUNZA, kwa sababu katika Karne hii Ya 21 kuna Maendeleo makubwa sana Ya Teknolojia na Ni ULIMWENGU WA TAARIFA hivyo usipojifunza kamwe hauwezi kuwa na Taarifa sa...

KURASA 05; KUJITAMBUA, Na umuhimu wake katika maisha ya kila siku

" Kujitambua"  maana  yake  nini?? Unaelewa  nini  kuhusiana  na  neno Hili Kujitambua?. ' Kujitambua '  limetokana  na  neno Tambua lenye maana ya kujua/kuelewa Hivyo; Kujitambua ni hali ya mtu binafsi kujielewa vile alivyo. Au uwezo wa mtu binafsi kung'amua yeye ni nani?, Anapaswa kufanya nini na kwa sababu ipi na lini? Pia, Kujitambua ni uwezo wa mtu  binafsi  kujielewa vizuri kuhusu yeye, tabia zake , majibu yake na vyote vile ambavyo vinamzunguka.  Katika suala hili ya kujitambua , mtu huyu lazima aweze kuyaelewa mambo yafuatayo kuhusu yeye ;  Yeye ni nani? (Mimi ni nani?) Uwezo wake (wako binafsi) ni upi?  Hapa naamanisha (upekee wako ulionao ) kunakopelekea utofauti wako na watu wengine Nini  natakiwa kukifanya hapa duniani? Unaelekea wapi ? Mchango wako  kwa jamii inayokuzunguka ni upi?? 👆 hayo ni mambo ambayo mtu anayejitambua ana...

KURASA 04; MAISHA NI MAAMUZI, Ukiamua unaweza kufanya jambo lolote lile utakalo

Habari rafiki mpendwa;  Ni matumaini Yangu u mzima wa afya na waendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Karibu sana katika Makala hii Ya Kurasa za Mafanikio,   Hakuna jambo chini ya jua ambalo linashindikana kufanyika. Ndani yetu ipo nguvu kubwa sana ambayo Mungu ameweka ndani  yetu.Na kama mtu ataijua nguvu kubwa iliyopo ndani yake , hakika anakwenda kuwa na Maisha mazuri sana. UKWELI KUHUSU WEWE. Unajidharau sana na wakati mwingine kudhani kwamba hauna thamani katika dunia hii.Na unadiriki kusema kwamba umezaliwa kwa bahati mbaya. Kufanya hivyo unajikosea na kujichelewesha mwenyewe,  Hakuna mwanadamu alizaliwa kwa bahati mbaya. Kila mmoja aliyepo katika dunia hii ameumbwa kwa kusudi Maalumu. Wewe ni wa thamani sana, na kuumbaa kwako duniani  kunadhihirisha kuwepo kwa jambo ambalo linakutaka wewe kulitimiza. Tambua ya kuwa wewe ni mtu wa  tofauti na hakuna anayefanana na wewe katika dunia hii.Na Vile wewe un...

KURASA 03; Kama unataka kufanikiwa , zingatia kitu hiki

Habari rafiki mpendwa,  Karibu sana kama makala hii ya Kurasa za Mafanikio  ili tujifunze na kupata mafanikio makubwa  Wakati tukiwa wadogo, wazazi walikuwa wanatukataza kucheza na kushirikiana na baadhi ya watoto/familia fulani, na endapo hutawasikiliza    unapata adhabu kubwa sana. Na walitukataza pia kutokula  katika familia hizo. Na zipo familia/watoto fulani ambao wazazi wanakuruhusu kwenda kucheza na kushirikiana nao na pengine wakakuruhusu kula chakula katika familia ile na hata kulala pale pale. Na sababu kubwa ilikuwa  ni kuhakikisha  hatuharibiki katika tabia zetu .Na Katazo hilo lilikuwa linakuja baada ya Kutoridhishwa na tabia za watoto hao. Jambo hili linaweza kutusaidia kujifunza machache kuhusu mchango wa wanaotuzunguka katika tabia zetu. Ukiambatana na mwenye tabia ya  wizi, bila shaka utajifunza kuhusu wizi . Ukiambatana na mwenye tabia ya Uongo, bila shaka nawe utakuwa na tabia hiyo hiyo. Uk...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...

KURASA 01; Hiki ndicho kinachokukwamisha usipate mafanikio.

Habari  yako  mpendwa, Natumai  u  mzima  na  unaendelea  na  majukumu yako  ya  kila  siku. Karibu  sana  tuweze  kujifunza  na  kupata  maarifa  ili  tuweze  kuwa  bora  zaidi  na  kuwa  na mafanikio  makubwa   katika  maisha  yetu . Hakuna  mtu  hata  mmoja  ambaye  anapenda kushindwa,  kila  mtu  anatamani  afanye  vizuri na apate  mafanikio  makubwa  sana. Hakuna  mtu  anayependa  kuwa  masikini,  kila mtu  anapenda  awe  tajiri  na  kufanikiwa  katika kila  jambo  analolipanga  kulifikia. Kila  mmoja  anapenda  kufikia  viwango  vya  juu sana  vya  mafanikio,  na  hata  wanafunzi  shuleni hakuna  anayetamani  kufeli katika...