Skip to main content

HEKIMA YA SIKU; Kila Jambo ulifanyalo lifanye kama wajibu na si kutegemea shukrani au kutambulika


Kila jambo unalolifanya, lifanye kama wajibu, na usifanye ukitegemea kutambuliwa, au kupewa shukrani.

Watu wengi  wanapata shida sana  pale ambapo wanafanya mambo mengi, na hakuna anayeonekana kuwashukuru kwa yale wanayoyafanya.

Unajitoa kwa nguvu zako kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

Fuatilia mifano hii michache ili uweze kupata kile ninachokimaanisha hapa;

Mfano  wa kwanza; Viongozi mbalimbali tulio nao, wanatumia muda wao mwingi na nguvu nyingi kuhakikisha wale wanaowaongoza wanafika pale wanapotakiwa kuwa.

Na  hakuna hata mmoja anayetambua mchango wao na nguvu zao walizotumia kuwaongoza.
Na pengine asiwepo hata mmoja wa kusema asante kwa yale wanayafanya.

Mfano wa Pili; kwenye mahusiano,unakuta boyfriend/girlfriend anafanya kila anachoweza ili kuboresha mahusiano yao, kumsaidia kwa kila hali/changamoto anayoipitia Lakini haoni mwenzie akimshukuru au kutambua kwa kile anakifanya.

Mfano wa tatu; Kazini kwako, unafanya kila kitu vile inavyotakiwa, labda kila siku unawahi kufika   kazini  na hakuna anayetambua mchango wako hapo kazini kwako.

Na pengine unaweza ukawa umefanya jambo kwa nguvu zako zote halafu anayekuja kutambuliwa kwa kukamilika jambo lile ni mtu mwingine tofauti na wewe uliyehusika.

Mfano wa nne; Wazazi wetu pia wanatumia nguvu nyingi sana na muda wao mwingi, mali zao na kila kitu kuhakikisha watoto wao wanasoma na kufikia maisha mazuri.
Lakini cha kushangaza, hakuna mtoto anayetambua ule  mchango mkubwa ambao wazazi wamefanya kwa watoto wao.

Mfano wa Mwisho; Unatuma jumbe kwa mtu fulani au, unampigia simu kila siku au kila wakati, lakini hutaona yeye amekutumia Ujumbe wowote au kukupigia simu.
Wewe unamtafuta kila siku na kila wakati , lakini yeye hana muda wa kukutafuta kabisa.

Kwa mifano hiyo hapo juu, bila shaka inaweza kuwa changamoto kwako na pengine kushindwa kuendelea kumtafuta au kufanya kile ulichokuwa unakifanya.

Na kama utakifanya ,basi utakifanya kwa nguvu ndogo na si katika ubora ule wa mwanzo.

Na usipojua nini cha kufanya, unaweza kuharibu kabisa mwelekeo wako na vile ambavyo hapo kabula ulikuwa unafanya.

Ili usiumie na kupata shida kwa yale ambapo huoni mtu anatambua kile unakifanya unatumia nguvu nyingi na muda mwingi lakini hakuna anayekuja kukushukuru au hata kusema ahsantee.

Yafahamu yafuatayo na kisha anza kuyafanyia kazi;

*️⃣ Usifanye jambo ili mtu fulani akutambue au mtu fulani aje  kukushukuru.

*️⃣ Jua kuwa kile unachokifanya ni wajibu wako, hivyo fanya ukijua kuwa ni wajibu wako.

*️⃣Sio wote wanaweza kutambua kile unachokifanya, lakini upo wakati watatambua kile ulichokuwa unakifanya.
Pengine utakuwa haupo mahali hapo ndipo watakapotambua umuhimu wako.

*️⃣Kufanya jambo ili utambuliwe na kupewa shukrani kuna athari kubwa zaidi, ikiwemo kupunguza nguvu ya kukifanya kile kitu, na kushindwa kufikia malengo yako uliyoyakusudia.

Yajue haya ili yaweze kukusaidia na kujua kuwa unatakiwa kufanya kama wajibu wako na sio kufanya ili utambuliwe na mtu fulani.

Mungu akubariki sana.

#Hekima Ya Siku.
ELIMU KITAA.
_____________________________________________________

Makala hii imeandikwa na; 
Joshua Golyama
golyamajoshua@gmail.com
+255 764 257 495 
elimukitaa2020.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...