Skip to main content

#Najifunza 03; Namna ya kujiengea nidhamu katika kufikiri kuliko sahihi(Clear thinking)



Zipo  kanuni  nyingi  sana  ambazo  Waandishi  wameandika  na    kufundisha   kuhusu  kufanikiwa  katika  kila jambo tunalolifanya, Kila  mmoja ameandika kwa  namna  ile  ambayo  ziliweza  kumsaidia.

Lakini  ipo  Kanuni  moja  na  Ya Msingi  sana  katika  safari  ya  Mafanikio  nayo  ni  NIDHAMU  BINAFSI.
Kanuni hii ni kama kanuni kiongozi ambayo bila ya kuwa nayo hatuwezi kufanikiwa .

Nidhamu  ni  tabia  ngumu   kuijenga  katika  maisha  ya  Mwanadamu  na  Pia  ni  tabia  ambayo ukiwa   nayo  unaweza  ukafanikiwa  kwa  Haraka sana.

'Nidhamu  ni  uwezo  wa  mtu  kufanya  jambo fulani  analopaswa   kulifanya   kwa  wakati  sahihi ikiwa  anapenda  au  hapendi. 
 Nidhamu  ni  nguvu  inayotusukuma  kuendelea zaidi.

Karibu  tujifunze  kwa  pamoja  kuhusu  namna gani  tunaweza   kujijengea  nidhamu  ya   kufikiri  kwa  usahihi  zaidi  katika  maisha  ya  Kila  siku.
Moja  ya  nidhamu  ngumu  kuijenga  katika  maisha   ni  nidhamu  ya  kufikiri.

Hapa  tunawapata  watu  wa  aina  tatu  kuhusu kufikiri;  wapo  wale  wanaofikiri, wapo  wanaofikiri  kuwa  wanafikiri,  na  wapo  ambao wako tayari kufa kuliko kufikiri.
Hivyo  kufikiri ni tabia ngumu  ambayo  watu  wengi  hatupendi kuifanya na wakati mwingi inatugharimu  sana  katika  kuchukua maamuzi , tunachukua  maamuzi  kulingana  na  hisia na si katika   uhalisia   wenyewe.

Fanya yafuatayo ili kujijengea nidhamu ya kufikiri kwa usahihi; 

  1. Pata muda wa kufikiri na kutafakari kuhusu mambo muhimu na matatizo mbalimbali unayokutana  nayo  katika  maisha. (hali  uliyo nayo  sasa
  2. Hakikisha  unapata  utulivu  wa  kutosha   kwa dakika  30-60   utumie   kwa  ajili  ya  kufikiri  na  kutafakari  kuhusu  mambo  mbalimbali.  Uwe  na desturi  ya   kukaa  peke  yako  kwa  muda  fulani, mahali  ambako   kuna  utulivu  wa  kutosha.
  3. Kukaa  peke  yako  na  kwa  utulivu mkubwa , huamsha   ufahamu  wako  na  kuweza  kuyaelewa mambo  mbalimbali  kwa  urahisi  zaidi  na  kufikia maamuzi   mazuri.
  4. Kulifanikisha  hili,  hakikisha   unakuwa  na  diary, notibuku au kidaftari kidogo   ambacho  unakitumia  kutunzia  Kumbukumbu,  andika  kila jambo  unalolipitia  katika  maisha   yako/hali  uliyo  nayo  kwa  sasa.  Na  kufanya  hivi  kunakusaidia sana kupata mawazo mapya yaliyo ya msingi sana .
  5. Aristotle  alisema  kuhusu  Hekima ( uwezo wa kuwa  maamuzi  mazuri)  ni   mjumuisho wa uzoefu na kutafakari(reflection). Kadiri  unavyotafakari  na  kufikiri  zaidi  kuhusu  uzoefu  wako,  ndipo  unapojifunza  zaidi   na  kuyafahamu mambo   mengi  zaidi.
  6. Fanya   mazoezi   kwa   dakika  30-60   kila  siku,  Wakati  unapoendelea   kufanya   mazoezi     unapopata    mawazo   mapya   na  kufanya maamuzi   mazuri. 

Hekima =  Uzoefu +  Kufikiri 

Ili  kuweza  kuchukua  maamuzi  yaliyo  bora zaidi(sahihi)  katika  maisha  yako  ni  lazima  uwe na  tabia  ya  Kufikiri  Kwa  umakini.
Watu  wengi  tunaendeshwa  na  hisia  na  si  kwa kufikiri  na  kufikia  maamuzi  sahihi


Hatua ya Kuchukua; 

Jenga  nidhamu  hii  ya  kukaa  peke  yako  na kufikiri  kwa  umakini  sana  kuhusu  maisha yako  na  jambo  lolote  unalotamani  kulifikia  katika maisha.  Unapokuwa  peke  yako  unapata  mawazo mapya  na  kufikia  hitimisho  lilio  sahihi  juu ya jambo  lolote.
Fikiri kabla ya kutenda, Usiendeshwe na hisia  bali chukua maamuzi yaliyo bora zaidi.

Maamuzi  ya  haraka  huwa  ni  maamuzi  yasiyo sahihi, 



#Najifunza. 
_____________________________________
Makala hii imeandikwa na ; 
Joshua Golyama, ambaye ni Mwalimu, Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo, Mhamasishaji Wa Mafanikio na Mwandishi.

+255 764 257 495 / +255 622 163 323
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com

Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...