Skip to main content

KURASA 04; MAISHA NI MAAMUZI, Ukiamua unaweza kufanya jambo lolote lile utakalo


Habari rafiki mpendwa; 

Ni matumaini Yangu u mzima wa afya na waendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.


Karibu sana katika Makala hii Ya Kurasa za Mafanikio,  

Hakuna jambo chini ya jua ambalo linashindikana kufanyika.
Ndani yetu ipo nguvu kubwa sana ambayo Mungu ameweka ndani  yetu.Na kama mtu ataijua nguvu kubwa iliyopo ndani yake , hakika anakwenda kuwa na Maisha mazuri sana.

UKWELI KUHUSU WEWE.
Unajidharau sana na wakati mwingine kudhani kwamba hauna thamani katika dunia hii.Na unadiriki kusema kwamba umezaliwa kwa bahati mbaya.

Kufanya hivyo unajikosea na kujichelewesha mwenyewe,  Hakuna mwanadamu alizaliwa kwa bahati mbaya.
Kila mmoja aliyepo katika dunia hii ameumbwa kwa kusudi Maalumu.

Wewe ni wa thamani sana, na kuumbaa kwako duniani  kunadhihirisha kuwepo kwa jambo ambalo linakutaka wewe kulitimiza.

Tambua ya kuwa wewe ni mtu wa  tofauti na hakuna anayefanana na wewe katika dunia hii.Na Vile wewe unajiona ni tofauti na uhalisia wako(vile Mungu anakuona)

Mungu kukuumba wewe alikuwa na Makusudi kamili na umezaliwa hapo ulipo, na vile ulivyo ni kutokana na mpango na makusudi yake Mungu.

Ndani yako kuna uwezo mkubwa sana, ambao ukiamua kuutumia unaweza kufanya mambo
makubwa sana katika dunia hii.
Usijidharau na kuanza kujiona kama hufai kuwepo duniani , hapana.

Upo duniani kulitimiza Kusudi La Mungu katika maisha yako.
Mungu alituumba ili tuweze kuwa Watawala, na tunatawala kupitia Vipaji na uwezo ambao  Mungu ametupa.

Katika makala ya leo tunakwenda kujifunza nguvu iliyopo katika maamuzi , 
Maisha ni maamuzi , ukiamua unaweza kufanya jambo lolote lile ulitakalo kulifanya na kulikamilisha.

Kila jambo linafanikiwa pale mtu anapoamua.
Licha ya kuwa na kanuni zingine za mafanikio/maisha ya kila siku, usipoamua kuzifanyia kazi  huwezi kufika popote 

Watu wengi tunatamani kufanya mambo mbalimbali katika maisha haya tuliyo nayo. Mwingine anatamani kuanza biashara , mwingine anatamani kulima , na mwingine kufuga na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Changamoto kubwa ni kwa sababu hatujaamua kufanya , tunatamani kufanya lakini hatujaamua kufanya.
Kutamani ni Msingi mkuu wa Mafanikio.
Lakini "Kutamani hakutakuwa na Maana pale tusipoamua"
Usipoamua na kuchukua hatua ya kuanzisha biashara,  hakuna biashara itakayofanyika
Usipoamua na  kuchukua hatua juu ya jambo fulani , kamwe hatuwezi  kufika kule tunataka kufika.

Kiwango cha Maisha yako, kinategemea na Umeamua yaweje, 
Ukitaka kuwa Masikini ni wewe tu kuamua 
Ukitaka utajiri ni wewe tu kuamua.
Maamuzi yako na wewe,  mhusika na bosi wa maisha yako ni wewe.
Hakuna mwingine mwenye dhamana na maisha yako.Usipoamua sasa kutafuta na kufanya bidii ili kuwa na  Maisha bora , hutamulaumu yeyote bali ni wewe mwenyewe.

Hauwezi kuwa bora katika fani fulani kama tu hujaamua kwa hivyo(bora)
Hauwezi kufaulu mtihani wako kama haujaamua kufaulu mtihani 
Hauwezi kuwa Tajiri kama tu haujaamua kuwa tajiri.

Hivyo amua sasa ni aina gani ya maisha unayahitaji, kiwango gani unataka kufanikiwa na fedha kiasi gani unataka kumiliki  n.k.
Na kisha AMUA kuvitafuta  kwa bidii zote na hakika utavipata .


Hatua Ya Kuchukua;

Usiishie tu kutamani, bali anza kuchukua hatua.
Amua kuwa bora, kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza kile ambacho ulitamani kifanyike katika maisha yako.
Kama kuna kitu unakitamani kukifanya katika maisha yako, amua na anza kukifanya.

Amua na chukua hatua ya Kujifunza zaidi ili kuweza kuwa bora zaidi katika kila jambo unalolifanya hapa duniani .


Ahsante sana kwa wakati wako.

Joshua Golyama .


_____________________________________
Makala hii imeandikwa na ; 
Joshua Golyama, ambaye ni Mwalimu, Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo, Mhamasishaji Wa Mafanikio na Mwandishi.

+255 764 257 495 / +255 622 163 323
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com
Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com




Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...