JENGA TABIA YA KUJIFUNZA KILA WAKATI , ONDOA KIBURI KATIKA KUJIFUNZA.
Unapokosa tabia ya kujifunza na kuwa na hali ya kujiona unajua kila kitu utakuwa nayo na Kwa Maana Hiyo hautaweza kuwa na spirit ya kuendelea kujifunza zaidi na zaidi.
Lakini unapokuwa unajifunza kila wakati, utagundua kwamba Mambo mengi huyajui hii itaamusha Nguvu mpya, ari mpya na hamasa ya kue ndelea kujifunza zaidi.
Jifunze zaidi ili upate hamasa ya kujifunza zaidi.
Na MUHIMU, ili uweze kujifunza ni lazima ujione hujui , na kama utaona kama unajua kamwe hautaweza kujifunza
Kwa maneno Mengine unakuwa na KIBURI KATIKA KUJIFUNZA ambacho Kinakuzuia wewe kujifunza zaidi, kwa sababu ndani yako kutakuwa na Sauti kama hii 'mbona kila kitu ninakijua, kujifunza ni kupoteza muda'
Hakikisha unajitahidi unakuwa na Tabia Ya KUJIFUNZA, kwa sababu katika Karne hii Ya 21 kuna Maendeleo makubwa sana Ya Teknolojia na Ni ULIMWENGU WA TAARIFA hivyo usipojifunza kamwe hauwezi kuwa na Taarifa sahihi za kukusaidia kuendana na kasi ya Maisha ya Ulimwengu wa sasa.
Zipo njia nyingi ambazo unaweza kujifunza
MOJA; Kwa kusoma Vitabu, kitu ambacho hujajua ni kwamba katika vitabu kuna Hazina kubwa sana, ambayo ni msaada sana kwako.
Kitu ambacho wewe hukifahamu , wapo wanaokifahamu na Wameandika kwenye Vitabu.
Hivyo, Anza kusoma vitabu ili uweze kuipata hazina ambayo imefichwa kwenye vitabu.
MBILI; Kupitia Changamoto unayoipitia au Changamoto ambayo watu wengine wanaipitia.
Kila changamoto inayotokea katika maisha yako ina darasa ndani yake, kuna kitu cha kujifunza
Kila changamoto inayotokea katika maisha yako ina darasa ndani yake, kuna kitu cha kujifunza
Tatizo ni kwamba watu wengi wanapopata changamoto, wanaitazama kwa upande mmoja na Si katika pande mbili,
Katika changamoto kuna Fursa ya kujifunza, na kuweza kubadili ufanyaji wa mambo na kazi yako.
Pia, changamoto ambazo watu wengine wanazipitia tunayo nafasi pia ya kujifunza kwa namna ambavyo wanakabiliana na changamoto wanazozipitia.
Bila shaka umepata kitu tayari kwa siku ya leo.
Jenga tabia Ya Kujifunza kila wakati na Kila siku.
See you shining and enjoying the cake!
Makala hii imeandikwa na;
Joshua Golyama (Mhamasishaji Na Mwandishi)
Whatsap number 0764 257495
Email; golyamajoshua@gmail.com
Whatsap number 0764 257495
Email; golyamajoshua@gmail.com
Comments
Post a Comment