Skip to main content

KITABU CHA JUMA; My Philosphy For Successful Living -Falsafa Yangu Ya Maisha Ya Mafanikio.



KITABU CHA JUMA; My Philosphy For Successful Living -Falsafa Yangu Ya Maisha Ya Mafanikio.

Habari ya kwako rafiki mpendwa,

Natumai umekuwa na wiki ya baraka sana na bila shaka umepiga hatua kadhaa zenye kukusaidia katika safari hii tuliyonayo ya kulikamilisha kusudi la Mungu katika maisha yetu.

Nikukaribishe katika makala hii ya kitabu cha Juma,  kutoka katika Kitabu Cha My Philosophy For Successful Living-Falasafa yangu ya Maisha Ya Mafanikio kilichoandikwa na Jim Rohn

Jim Rohn ni Mjasiriamali wa Marekani, Mwandishi, na mhamasishaji
Katika Juma hili tunakwenda kujifunza mambo machache na ya muhimu sana kutoka katika Kitabu hiki  cha My Philosophy For successful living

Karibu sana tujifunze kwa pamoja mambo haya ambayo mwandishi anatufundisha katika kitabu hiki

Kila mmoja wetu anatamani kuwa na maisha mazuri, hakuna hata mmoja anayetamani kuishi maisha ya shida.
Lakini kutokana na ujinga wetu wa kutofahamu kanuni za Msingi za kuwa na maisha mazuri tunaishia kuhangaika tu na kupata shida zaidi.

Katika kitabu hiki cha juma tunakwenda kujifunza mambo Kumi ambayo ukiyaelewa na kuchukua hatua tutakuwa na maisha bora sana.

 Mambo kumi ya Kujifunza kutoka katika kitabu cha My pPhilosophy For Successful living.

1.Muda ni wa thamani sana kuliko fedha, unaweza kupata fedha kila siku na kila siku, lakini muda hauwezi kuupata
Ukishapoteza muda hauwezi kuupata tena
Hivyo unatakiwa kuutumia muda unaoupata vizuri na kwa umakini mkubwa zaidi.

Epuka kupoteza muda kwa kuachana na kutofanya yale yasiyo na umuhimu kwetu.Maana wengi tunahangaika na mambo mengi sana ambayo hayana mchango wowote katika maisha yetu.

Pale  upatapo nafasi ya kufanya jambo lolote lile hakikisha unalikamilisha na kwa usahihi kabla ya kuanza kufanya jambo jingine.

2.Moja ya matumizi mazuri ya muda ni kuwekeza ndani yako binafsi (self-investment for self-development).

Kwa kusoma vitabu, Kujifunza kila wakati na kila siku, kuangalia na kusikiliza   picha za video zenye  mafundisho, kusikiliza audio zenye kukupa mafundisho mazuri (maarifa na yenye kukujenga), Hudhuria semina mbalimbali zinazofundisha  mambo mbalimbali kuhusu maisha.

NB; KUWA MAKINI SANA katika kuchagua vitabu sahihi vya kuvisoma.

3.Kujifunza ni mchakato (learning is the process).Safari ya kujifunza ni safari yenye mchakato , unakuwa unajifunza hatua kwa hatua, vipande vipande.Hauwezi kujifunza yote kwa siku moja.Hivyo usiache kujifunza

4.Wahirikishe wengine maarifa yale unayoyapata katika kujifunza.Ni muhimu sana kufanya hivyo kwa sababu Mambo mawili muhimu hutokea wakati unawashirikisha wengine maarifa uliyo nayo

   A. Kujifunza zaidi kwa yule anayeshirikishwa
   B.Anayeshikisha maarifa hayo kujifunza zaidi
Hivyo pale unapojifunza, chukua hatua na kisha washirikishe wengine yale uliyojifunza.

5. Si mambo yote unayojifunza yatakufaa kwa siku hiyo.Hata kama unaona hayakufai kwa sasa, yupo mtu mwingine ambaye yanaweza kumfaa, Lakini pia haujui ni lini hayo unayojifunza yatakuwa msaada katika maisha yako.
Hivyo, jifunze kila siku na yahifadhi kwa faida ya baadaye.

6. Elimu ya darasani (formal education) inakusaidia kupata ajira , lakini elimu binafsi  (Self-education)  ndiyo inayoweza kukufanya kuwa tajiri,
Elimu binafsi ni ile mtu binafsi kujisomea na kujifunza zaidi yeye mwenyewe, kwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina.


7. Siri kubwa ya Mafanikio imefichwa katika kuwasaidia wengine
Zig Ziglar anasema" Kama utawasaidia wengi wengi kupata kile wanachokihitaji katika maisha yao, unaweza kupata chochote kile unachokihitaji

  "If you help enough people get what they want, you can get everything you want"__Zig Ziglar

Tafuta kila njia na namna mbalimbali za kuwasaidia watu wengi zaidi
Kufikia mafanikio makubwa , utajiri na kupata chochote kile kimefichwa katika kuwasaidia wengine.
Pale wengine wanapofanikiwa nawe unaweza kufanikiwa na  kupata chochote kile unachokihitaji.

Fikiria nini cha kuwafanyia wengine , familia yako, ndugu zako,jirani zako,  Dola yako, nchi na ulimwengu pia.

8. " Fedha ni mchezo wa thamani" Kadiri unavyotoa thamani , ndivyo unavyoweza kulipwa zaidi
Unalipwa kutokana na kile unachokipelea sokoni na thamani  yake ikoje, na Mchango wako wako unaoutoa kwa kazi/jambo lolote ulifanyalo, hutabiri ni kiwango gani cha fedha utakacholipwa
Hivyo katika kazi zetu, biashara zetu, cha msingi ni kutafuta kuongeza thamani zaidi katika vile unavyovifanya.

Kiwango cha fedha unacholipwa kutokana na jambo fulani ni thamani yako unayoitoa katika jambo hilo.

9. Unahitaji falsafa bora ili kuweza kuendesha maisha yako.Kila jambo lina mwongozo wake
Ubora wa falsafa ndio unatabiri aina ya mafanikio unayokwenda kuwa nayo.

Hakuna kitakachobadilika,hadi  pale utakapobadilisha falsafa yako, .
Jim Rohn anasema ili kuwa na fedha/kutengezea pesa kunaanzia kuwa na falsafa sahihi/bora inayokuongoza

Angalia falsafa hizi mbili;

(a) Tumia kwanza, kisha wekeza fedha inayobaki
(b) Wekeza, na kisha tumia fedha inayobaki
Falsafa ya (a) itakupeleka kuwa masikini , maana yake sio falsafa sahihi kama unataka kufanikiwa.
Falsafa ya (b) ni sahihi na ukiitumia unakwena kufanikiwa.

10. Mambo matano Muhimu ili kuwa na maisha ya mafanikio.

A.Chagua watu sahihi kuambatana nao, katika safari hii uliyo nayo.Wale wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana katika tabia yako, na maisha yako kiujumla.Hivyo unatakiwa kuwa makini sana na wale wanaokuzunguka na unaoambatana nao.

B.Jifunze kuwa na lugha nzuri kwa wafanyakazi wako na wote unaowahudumia.
Hakikisha unawasiliana nao vizuri sana na Kama inawezekana jifunze lugha zaidi ya tatu ili kuweza kuboresha huduma zako na mawasiliano yako

C.Fikiria zaidi kuzalisha/kuja na kitu chenye thamani sana kwa ulimwengu., Kila kitu unachokifanya hakikisha unakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana ili kuhakikisha kila kitu ukifanyacho kinakuwa na thamani kwa wote na ulimwengu pia.

D.Jenga na Imarisha mausiano yako
Yape thamani mahusiano uliyo nayo na watu, mfano marafiki zako.Washirikishe kile unachokifanya na wahamasishe zaidi waweze kuchukua hatua zaidi.

Na hii itakusaidia pale utakapokutana changamoto mbalimbali watakuhamasisha na kuhakikisha unaendeleza kazi unayoifanya

E. Mungu ndio msingi wa Kila kitu, hakikisha kila unalolifanya unamshirikisha Mungu na kuwomba Mungu aweze kutembea na wewe ili kulifanikisha lile umekusudia.

Hayo ndiyo mambo kumi kati ya mengi zaidi ambayo tunajifunza kutoka katika kitabu hiki .

Natumai umejifunza mambo mengi, hivyo nikusihi kuchukua hatua kwa kuyatendea kazi zaidi.

Kupata uchambuzi zaidi tembelea mtandao wa ELIMU KITA elimukitaa2020.blogspot.com huko utapata ufafanuzi kwa undani  zaidi juu ya kitabu

Kujiunga na Group La ELIMU KITAA tuma sms kwa njia ya whatsap ikiwa na Jina Lako pamoja na Neno NIUNGE ELIMU KITAA nawe utaunganishwa.

Ahsante sana.

Wako
Joshua  Golyama
Simu; +255 764 257 495
golyamajoshua@gmail.com/elimukitaa2020@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...