Skip to main content

Posts

KUTOA KAFARA ILI UWEZE KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA.

Bila shaka kichwa cha mada hii kinakuchanganya na unashindwa kuelewa nini nimedhamiria  kukuambia, Lakini ambatana nami hadi mwisho mwa Makala hii utaelewa maeneo halisi ya mada hii ya leo. Karibu sana tujifunze pamoja ili tupate Maarifa ya kutusaidia. Wakati naendelea kusoma vitabu mbalimbali, nilikutana na jambo hili ambalo lilinishangaza kidogo, lakini nilijifunza mambo mengi sana muhimu katika safari ya mafanikio. Nimeyasoma na kujifunza kutoka kitabu cha K WANINI HADI WEWE SIO TAJIRI   kilichoandikwa na Kocha Makirita Amani Nimeamua nikushirikishe maarifa haya nawe upate kujifunza , na kuchukua hatua ya kuyafanyia kazi. Mwandishi anaanza kwa kueleza yafuatayo;  Huwezi kufikia utajiri mkubwa na mafanikio kwenye maisha bila ya KUTOA KAFARA. Mwandishi anaeleza dhana ya TRADE OFF akiwa na maana kwamba " Kupoteza kitu fulani ili kupata kitu kingine , au kuliwa eneo fulani ili uweze kula eneo jingine  Kafara anayozungumzia mwandishi...

KITABU CHA JUMA; My philosophy for successful living-Falsafa Yangu ya Maisha Ya Mafanikio Kilichoandikwa na Jim Rohn

KITABU CHA JUMA;  My philosophy for successful living- Falsafa Yangu ya Maisha Ya Mafanikio  Kilichoandikwa na Jim Rohn. Moja ya jambo muhimu sana katika dunia hii ya sasa ni kujifunza, ili kuweza kuwa bora zaidi katika jambo lolote huna budi kuwa na tabia ya kujifunza,  Kupitia kujifunza tunapata maarifa ambayo yanaweza kutuvusha hatua moja kwenda hatua nyingine. Kufikia mafanikio makubwa sana katika maisha hatuna budi kujifunza kila siku Watu wengi ambao wamefanikiwa wana tabia moja muhimu sana ambayo ni Kujifunza kila wakati na kila siku, shauku yao kubwa ni kujfunza na kujua mambo mengi ambayo yanawasaidia kukua zaidi  Kupitia kujifunza, unapata nafasi ya kuyajua mambo mengi sana katika maisha.Hatuwezi kuyajua yote lakini tunatakiwa kujua mambo mengi. Kama utapata nafasi ya kuwafutilia sana wale wanaojua mambo mengi katika Jamii , wana tabia ya kujifunza kila siku na kila wakati. Hivyo, kama tunataka kufikia mafanikio makubw...

KARIBU KATIKA MTANDAO WA ELIMU KITAA (STREET EDUCATION); Tujifunze kwa pamoja, ili tupate maarifa sahihi ya kutusaidia katika maisha yetu.

                                                  Rafiki yangu mpendwa; Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na majukumu ya kila siku na unaendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuwa na maisha bora sana. Moja ya kitu cha msingi sana katika maisha ambacho hutakiwi kukiacha ni kujifunza kila siku na kutafuta kuwa bora zaidi. Maisha ni sanaa, na kama ilivyo sanaa inahitaji ubunifu kila siku, usipotaka kujifunza kamwe hauwezi kuwa mbunifu. Hivyo, katika maisha hutakiwi kuacha kujifunza ili uweze kuwa bora zaidi. Karibu sana katika Makala hii ambayo ni muhimu sana kwako na nimeifanya kuwa maalumu sana, kwa sababu nimekuandalia na kukuletea Makala hii ili uweze kujua hasa kwa undani kuhusu Mtandao huu wa Elimu KItaa (Street Education) chanzo chake, unahusika na nini, malengo yake na nini utakipata katika mtandao huu. Karibu s...

KURASA 05; KUJITAMBUA, Na umuhimu wake katika maisha ya kila siku

" Kujitambua"  maana  yake  nini?? Unaelewa  nini  kuhusiana  na  neno Hili Kujitambua?. ' Kujitambua '  limetokana  na  neno Tambua lenye maana ya kujua/kuelewa Hivyo; Kujitambua ni hali ya mtu binafsi kujielewa vile alivyo. Au uwezo wa mtu binafsi kung'amua yeye ni nani?, Anapaswa kufanya nini na kwa sababu ipi na lini? Pia, Kujitambua ni uwezo wa mtu  binafsi  kujielewa vizuri kuhusu yeye, tabia zake , majibu yake na vyote vile ambavyo vinamzunguka.  Katika suala hili ya kujitambua , mtu huyu lazima aweze kuyaelewa mambo yafuatayo kuhusu yeye ;  Yeye ni nani? (Mimi ni nani?) Uwezo wake (wako binafsi) ni upi?  Hapa naamanisha (upekee wako ulionao ) kunakopelekea utofauti wako na watu wengine Nini  natakiwa kukifanya hapa duniani? Unaelekea wapi ? Mchango wako  kwa jamii inayokuzunguka ni upi?? 👆 hayo ni mambo ambayo mtu anayejitambua ana...

Ifahamu siri hii ili uweze kufanikiwa zaidi katika maisha yako

Je, umewahi kujiuliza kwanini watu wengi wanaanza biashara na baada ya muda mfupi wanaacha? Na Kwanini biashara za watu fulani zinakuwa na wateja wengi kuliko biashara zingine  Nini siri ya Haya yote? Karibu tujifunze kwa pamoja ili tupate  majibu ya maswali yetu tunayojiuliza . Jibu la swali letu kwa nini biashara nyingi zinakosa wateja na zingine kuwa na wateja wengi ni UBORA na THAMANI inayotolewa na Biashara husika. Katika biashara yoyote ile yako mambo mawili makubwa ambayo wateja wanayaangalia. 1.Unafuu wa bei 2.Ubora wake. Wateja wanataka kitu  chenye bei rahisi na pia ambacho kina ubora. Ukweli ni kwamba katika nyakati hizi za utandawazi  hakuna baishara mpya  au chochote kipya ambacho unaweza kukifanya. Karibia kila kitu wapo watu wanakifanya. Na hauwezi ukasema kwamba unaenda kufanya jambo jipya kabisa ambalo halijwahi kufanyika   Kila kitu/biashara wapo watu wanaoifanya baishara hiyo.Hivyo hauko p...

#Najifunza 04; Liko kundi nyuma yako linakufuatilia vile unavyoenenda(mwenendo)

Nyuma Yako liko kundi kubwa sana  la watu wanaojifunza kutoka kwako,  Yaani wanafuata vile wewe unavyofanya . Ukifanya , nao wanafanya na Usipofanya nao hawafanyi pia Ki-ufupi wewe Ni Kiongozi wa Kundi kubwa sana La Watu USILOLIJUA . Hivyo pale unapoacha kufanya Kile ulichoanza kufanya,  Unapo KATA TAMAA ,  na wao pia wanashindwa kuendelea kwa sababu  kiongozi wao  umekata Tamaa. Usikate Tamaa,  Usivujike Moyo na Kurudi Nyuma ,  Kwani lipo Kundi kubwa  La watu usilolijua wanaanguka baada Ya wewe KUKATA TAMAA. Usikate Tamaa , Songa Mbele na Fanya Kiume Uwe Hodari Kwa FAIDA YAKO na WALE WOTE WANAOJIFUNZA KUTOKA KWAKO( KUNDI KUBWA LA WATU USILOLIJUA ) . Kabla Hujakata TAMAA, Kurudi Nyuma na Kuacha Kabisa KUMBUKA hili , itakusaidia Kuendelea Mbele zaidi. Kwa kuwa lipo kundi kubwa linakufuatilia, fanya vile bora na kwa umakini wa hali  ya juu sana. Usikate tamaa, Songa mbele kwa ajili ya Faida ya Wengine, hata kam...

KURASA 04; MAISHA NI MAAMUZI, Ukiamua unaweza kufanya jambo lolote lile utakalo

Habari rafiki mpendwa;  Ni matumaini Yangu u mzima wa afya na waendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Karibu sana katika Makala hii Ya Kurasa za Mafanikio,   Hakuna jambo chini ya jua ambalo linashindikana kufanyika. Ndani yetu ipo nguvu kubwa sana ambayo Mungu ameweka ndani  yetu.Na kama mtu ataijua nguvu kubwa iliyopo ndani yake , hakika anakwenda kuwa na Maisha mazuri sana. UKWELI KUHUSU WEWE. Unajidharau sana na wakati mwingine kudhani kwamba hauna thamani katika dunia hii.Na unadiriki kusema kwamba umezaliwa kwa bahati mbaya. Kufanya hivyo unajikosea na kujichelewesha mwenyewe,  Hakuna mwanadamu alizaliwa kwa bahati mbaya. Kila mmoja aliyepo katika dunia hii ameumbwa kwa kusudi Maalumu. Wewe ni wa thamani sana, na kuumbaa kwako duniani  kunadhihirisha kuwepo kwa jambo ambalo linakutaka wewe kulitimiza. Tambua ya kuwa wewe ni mtu wa  tofauti na hakuna anayefanana na wewe katika dunia hii.Na Vile wewe un...