Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2020

#Najifunza 02; Huu ndio wakati sahihi wa kumjua vile mtu alivyo

Maisha ya Mwanadam yamejaa maigizo , na wengi wao hawapendi kuishi maisha yao(uhalisia wao). Na kwa namna hii huwezi kufahamu mtu kwa undani vile alivyo.Kwa sababu anaweza kuigiza maisha yasiyo yake na ukamwamini. Lakini Wakati mzuri wa kumjua mtu vile alivyo ni pale anapopitia changamoto kubwa katika maisha yake. Hapo ndipo uhalisia wake huonekana, uimara wake, nguvu zake, akili zake na yote yanayomhusu  Mwanafalsafa(Mstoa) aliwahi kusema maneno haya,  " Difficulties are things that show a person what they are" __ Epictetus Akiwa na maana hii kwamba,  magumu ni mambo ambayo yanamwonesha mtu jinsi alivyo. Zinapofika nyakati ngumu , ndipo ambapo tunaweza kumjua mtu vizuri na hiki ndicho kipondi kizuri sana ambacho kinamwonesha mtu vile alivyo. Kwa sababu wakati wa Raha mtu anaweza kuigiza na akafanikiwa kufanya hivyo. Ili kudhibitiisha uimara wako/kwamba umeimarika ni lazima magumu/changamoto uzipate ili kudhibitisha hi...

#Najifunza 01; Muda ni muchache, Usiige maisha ya watu wengine, Ishi maisha yako.

Nukuu kutoka kwa Steve Jobs. " Our time is limited, so don't waste it living some one else's life.Do not be trapped by dogonas means living by using other people's thoughts , Don't let the noise of other people's opinion muffle your inner voice The most important thing that have courage to follow your heart and mind some how they already know what  you really must become .Every thing is of secondary importance". Machache tunayojifunza kutoka katika Nukuu hii ni haya;    Muda wetu tulio nao ni mchache sana na yapo mengi sana ambayo yanatusubiri tuweze  kuyafanya.Tunapaswa kuwa Makini sana  tunapoendelea kwani Muda ni mchache.     Kwa kuwa muda muchache sana , tusiupoteze kwa kuishi maisha ya watu wengine. Tusiige maisha ya watu wengine, kila mmoja aishi maisha yake.       Fanya kile unachokiamini kwamba ni sahihi na kinakuletea Matokeo chanya katika maisha yako.       Usiishi kwa kufuata ...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...

KURASA 01; Hiki ndicho kinachokukwamisha usipate mafanikio.

Habari  yako  mpendwa, Natumai  u  mzima  na  unaendelea  na  majukumu yako  ya  kila  siku. Karibu  sana  tuweze  kujifunza  na  kupata  maarifa  ili  tuweze  kuwa  bora  zaidi  na  kuwa  na mafanikio  makubwa   katika  maisha  yetu . Hakuna  mtu  hata  mmoja  ambaye  anapenda kushindwa,  kila  mtu  anatamani  afanye  vizuri na apate  mafanikio  makubwa  sana. Hakuna  mtu  anayependa  kuwa  masikini,  kila mtu  anapenda  awe  tajiri  na  kufanikiwa  katika kila  jambo  analolipanga  kulifikia. Kila  mmoja  anapenda  kufikia  viwango  vya  juu sana  vya  mafanikio,  na  hata  wanafunzi  shuleni hakuna  anayetamani  kufeli katika...

AFYA; FAHAMU KUHUSU PARACHICHI NA UMUHIMU WAKE MWILINI

FAHAMU KUHUSU PARACHICHI NA UMUHIMU WAKE MWILINI  Habari yako  mpendwa, Ni matumaini yangu kwamba u mzima na waendelea vyema na maisha ya kila siku, huku ukitafuta na kunia kufikia mafanikio makubwa sana maishani mwako. Karibu sana tuweze kujifunza kuhusu Afya, na leo tunaangalia tunda linaloitwa  parachichi pamoja na umuhimu katika mwili wa Mwanadamu. Miongoni mwa vyakula vinavyohitajika ili kukamilisha mlo kamili ni MATUNDA, matunda hutupatia faida nyingi sana katika miili yetu .Yapo matunda mengi sana na yote yana faida kubwa sana katika Mwili wa  Mwanadam. Leo tunakwenda kufahamu kiundani kuhusu Parachichi na faida zake katika Mwili wa Mwanadamu. Karibu sana ndugu yangu tujifunze na tuanze kulitumia tunda hili baada ya kujua faida nyingi tuzipatazo wakati tunatumia tunda hili    Parachichi (avocado) Persea americana Tunda aina ya parachichi hujulikana kama embefuta kwa sababu limejaa mafuta yenye faida nyingi sana katika afya ya mwan...

AGRICULTURE 101; UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI

Habari rafiki mpendwa; Ni matumaini yangu u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku , hongera kwa yote na endelea zaidi ili tuweze kufikia mafanikio makubwa zaidi Karibu sana katika mtandao huu wa ELIMU KITAA(STREET EDUCATION) ambao unahusika na kutoa elimu kwa njia ya makala kuhusu mambo mbalimbali kama vile , Kilimo,  Afya,  ufugaji, Mafanikio binafsi , na makala zinazoelimisha zaidi kuhusu kulijua Kusudi la Mungu katika maisha yako, pia Mtandao huu unahusika pia kutoa makala zinazohusu Elimu ya Lishe na Matumizi ya Muda. Lengo kuu la mtandao huu ni kushirikisha na kutoa maarifa sahihi kwa watu wote kuhusu maduala yote tunayokutana nayo katika maisha. Huo ni utangulizi kiufupi kuhusu mtandao huu , Sasa nikukaribishe katika makala Ya AGRICULTURE 101 , ukurasa unaohusu masuala yot yanayohusu kilimo na mifugo, Leo tunakwenda kujifunza kiufupi kuhusu ufugaji bora kwa Kuku wa Mayai . Katika ufugaji wa aina mbili ambao unajulikana na kila mtu , ufugaji ...

HAKUNA ANAYEIJUA KESHO;Hili ni Fumbo Tulilofumbiwa Wanadamu

  Habari yako Rafiki Yangu Mpendwa; Hakuna hata mmoja katika dunia anayeijua kesho yake, hata wasomi, wanasayansi na wataalam wote hapa duniani hili ni fumbo kubwa sana ambalo Mungu ametufumba sisi wanadam kesho yetu ni fumbo , na hakuna anayejua pia baada ya sekunde moja, dakika moja , siku moja au miaka kadhaa inayo kitatokea kitu gani? HAKUNA KABISA anayejua  kesho au muda muchache ujao nini kitatokea. Fumbo hili linatufundisha mambo mengi sana, na kutupa tahadhari kuhusu maisha yetu na mipango/malengo yetu  tunayokuwa nayo. Na fumbo hili linatupa mwongozo na hekima zaidi juu ya mambo tuyafanyayo . Jifunze mambo yafuatayo na yatendee kazi , ukizingatia kwamba HAKUNA anayeijua kesho au muda muchache ujao nini kinaweza kutokea katika maisha yake    1. Usisubiri hadi uwe tayari ili kuanza kutimiza kusudi lako . Anza hivyo hivyo ulivyo  hata kama haujakamilisha mambo yote yanayohitajika .Hii itakusaidia  na Kuishinda roho ya kukata ta...

TUMIA MUDA WAKO VIZURI, CHAGUA MAMBO MACHACHE NA UYAFANYE HAYO

Habari ya kwako rafiki na ndugu yangu Mpendwa, Natumai u mzima na unaendelea vyema na majukumu ya Kila siku , nikukaribishe sana katika Makala hii ili tuweze kujifunza na kuweza kuwa bora katika maisha yetu. Tunatakiwa kufanya kazi, na vyote tuvifanyavyo kwa bidii , lakini sio kwa bidii tu bali KATIKA UBORA . Makala hii inaeleza namna gani tunavyoweza kutumia muda wetu vizuri, Watu wengi hulalamika sana na wakati mwingine kuwalaumu watu wengine kwamba wanawapotezea Muda wao, lakini kumbe hawajajua , hutakiwi kumlaumu mtu yeyote, anza wewe mwenyewe Wewe ndio chanzo kikubwa sana cha kupoteza muda Mpendwa upo msemo unaosema "mambo mengi muda muchache" msemo huu umekuwa maarufu sana , na wakati mwingine umekuwa unatumika kama sababu ya kuitumia pale anapoona anashindwa kuyafanya yale anayotamani kuyafanya .Muda upo mwingi sana , na ukweli ni kwamba "hakuna muda wa kutosha kufanya kila kitu , ila upo muda wa kutosha sana kufanya yale ya muhimu zaidi. Hivyo karibu tuj...