Skip to main content

#Najifunza 01; Muda ni muchache, Usiige maisha ya watu wengine, Ishi maisha yako.

Nukuu kutoka kwa Steve Jobs.

" Our time is limited, so don't waste it living some one else's life.Do not be trapped by dogonas means living by using other people's thoughts , Don't let the noise of other people's opinion muffle your inner voice
The most important thing that have courage to follow your heart and mind some how they already know what  you really must become .Every thing is of secondary importance".

Machache tunayojifunza kutoka katika Nukuu hii ni haya;
   Muda wetu tulio nao ni mchache sana na yapo mengi sana ambayo yanatusubiri tuweze  kuyafanya.Tunapaswa kuwa Makini sana  tunapoendelea kwani Muda ni mchache.
    Kwa kuwa muda muchache sana , tusiupoteze kwa kuishi maisha ya watu wengine. Tusiige maisha ya watu wengine, kila mmoja aishi maisha yake.
      Fanya kile unachokiamini kwamba ni sahihi na kinakuletea Matokeo chanya katika maisha yako.

      Usiishi kwa kufuata maoni/mapendekezo na mawazo ya watu wengine.  Maneno ya watu yasikufanye ukaenda kinyume na kile unachokiamini katika Maisha Yako.

      Jiamini wewe mwenyewe, Fuata kile akili yako na moyo wako vinakusukuma kufanya. Usifuate ushauri wa watu juu Ya Kile unachotaka kukifanya katika maisha yako.

ANGALIZO; Ushauri ni wa Muhimu sana, lakini sio kila Jambo unaweza kuomba ushauri. 
Mfano; kama hujui nini cha kufanya kama vile kazi au biashara, usiombe ushauri kabisa .
Jua kwanza Biashara au Kazi gani unataka ndipo uombe ushauri .
Na mara upatapo ushauri huo,  uchunguze kwa Makini ili kuona kama unaweza kukusaidia.UNATAKIWA KUWA MAKINI SANA HAPA.

Jambo La Muhimu zaidi ;  Kujua hasa nini unataka au kuwa nani? Mengine yote yanafuatia baada ya hili la kwanza.
Jua kule unakokwenda,  na vile unavyojiona  hapo baadaye.



#Najifunza. 
_____________________________________
Makala hii imeandikwa na ; 
Joshua Golyama, ambaye ni Mwalimu, Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo, Mhamasishaji Wa Mafanikio na Mwandishi.

+255 764 257 495 / +255 622 163 323
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com
Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...