Skip to main content

HAKUNA ANAYEIJUA KESHO;Hili ni Fumbo Tulilofumbiwa Wanadamu







 

Habari yako Rafiki Yangu Mpendwa;

Hakuna hata mmoja katika dunia anayeijua kesho yake, hata wasomi, wanasayansi na wataalam wote hapa duniani hili ni fumbo kubwa sana ambalo Mungu ametufumba sisi wanadam kesho yetu ni fumbo , na hakuna anayejua pia baada ya sekunde moja, dakika moja , siku moja au miaka kadhaa inayo kitatokea kitu gani? HAKUNA KABISA anayejua  kesho au muda muchache ujao nini kitatokea.

Fumbo hili linatufundisha mambo mengi sana, na kutupa tahadhari kuhusu maisha yetu na mipango/malengo yetu  tunayokuwa nayo.
Na fumbo hili linatupa mwongozo na hekima zaidi juu ya mambo tuyafanyayo .

Jifunze mambo yafuatayo na yatendee kazi , ukizingatia kwamba HAKUNA anayeijua kesho au muda muchache ujao nini kinaweza kutokea katika maisha yake


   1. Usisubiri hadi uwe tayari ili kuanza kutimiza kusudi lako .
Anza hivyo hivyo ulivyo  hata kama haujakamilisha mambo yote yanayohitajika .Hii itakusaidia  na Kuishinda roho ya kukata tamaa.
 KUMBUKA; muda huu haukusubiri wewe ili uwe tayari,  kadiri upatavyo nafasi , tumia vyema nafasi hiyo uliyoipata na nguvu zako zote


 2.Hakikisha unatumia Muda vizuri ili usije kujuta hapo baadaye na kuanza kusema kuwa Muda ni Mchache.  " Mambo mengi muda muchache"
Shughulika na wekeza nguvu zako zote  kwa mambo machache yaliyo na umuhimu kwako ili kuzuia kupoteza muda  kwa mambo mengi yasiyo na umuhimu kwako.


  3 .Fanya kazi kwa bidii na kwa ubora wa hali ya juu  sana kwa kila ukifanyacho.
 Fanya kazi kama ndiyo siku yako ya mwisho kuishi duniani _ Hii itakusaidia na kukuhamasisha Kusonga mbele zaidi .


 4.Ishi leo kwa kuwa hujui kesho yako itakavyokuwa Leo yako unaifahamu na kesho yako huijui,hivyo itumie leo yako vyema.Usiseme  nitaanza kesho HAPANA,  anza leo na usisubiri Kesho Kwa maana huna uhakika nayo.Muda sahihi na muafaka wa Kutimiza malengo yako ni SASA na siyo baadaye au kesho.


  5.Maisha hayakusubiri wewe ili uwe tayari , Maisha Yataendelea kwenda,  dunia itaendelea kwenda kwa sababu haijali kama upo tayari au umeshakuwa tayari.
Anza kidogo na kile ulichonacho, kuanza ni bora kuliko kuanza kabisa.Usiseme kwamba ngoja nisubiri hadi nitakapokuwa na Umri fulani.Muda na maisha havikusubiri wewe kuwa tayari
Anza kidogo kidogo huku ukishafanya kwa Umakini, na uaminifu mkubwa.
Hakuna mtu yeyote  aliyefanikiwa, aliyeibuka na kuwa na mafanikio hayo aliyonayo, bila shaka alianza mbali  sana kuwa kuanza kidogo kidogo na kufanya kazi kwa bidii, hatimaye kufika hapo walipofikia.


  6.Kama kuna kitu/jambo ambacho unatakiwa kuwa na UBAHILI nacho, basi ni muda wetu.
Watu wengi tumekuwa tunaruhusu mtu yeyote kutumia muda wetu, na kuanza kuwalalamikia wengine kwamba wanatupotezea Muda.Hupaswi kumlaumu mtu yeyote yule, kabla kuwalaumu wengine jlaumu wewe mwenyewe kwanza kwa kutokuwa makini na muda ulionao.
Wengi wetu tunautumia muda vibaya (hovyo)hasa kwenye starehe.
Kuwa BAHILI wa muda usiruhusu mtu yeyote kuutumia muda wako kwa namna yeyote ile.Tumia muda wako katika mambo ya muhimu na Msingi sana katika maisha yako.


  7. Ishi leo kama ndiyo siku yako ya mwisho;
 Chukulia kila siku kama ya mwisho , fanya yale ya muhimu pekee Maana *IPO SIKU HAITAKUWA NA KESHO. Hivyo usiseme nitafanya  KESHO  fanya SASA.


  8. Kuahirisha mambo ni moja ya upotevu wa muda,
Watu wengi huwa tunaahirisha  mambo yale ambayo tumeyapanga bila kujua madhara yake. Unapoahirisha kufanya unakuwa unapoteza muda kwa  sababu unapoahirisha kitu(jambo) siyo tu unapoteza muda wa SASA, bali unapoteza na muda ujao ambao huna uhakika nao.

Hivyo, ni vyema sana ukajitahidi kulifanya jambo ambalo umelikusudia kulifanya na usipende kuahirisha kila jambo unalolipanga.Hakikisha huruhusu sababu yoyote kukufanya uahirishe jambo ulilolikusudia.

Chagua sasa yale mambo yaliyo ya muhimu na umuhimu mkubwa kwako na tumia nguvu , juhudi na muda wote kushughulika nayo.

Mwisho; tunaposoma Maandiko Matakatifu tunapata jambo kubwa sana ambalo linakamilisha makala hii ya leo

 Mhubiri 9:10  "Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe."

Kila jambo unalolifanya lifanye kwa nguvu zako zote, na utafanikiwa.
Mungu akubariki sana.
Ahsante.


Makala hii Imeandikwa na;
 Joshua Golyama
Mwanafunzi Wa shahada Ya awali ya Sayansi Ya Kilimo
Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA-MOROGORO)
+255764257495
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com.
Blogs; elimukitaa2020.blogspot.comHakuna anayeijua Kesho;Hili ni fumbo tulilofumbiwa wanadam

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...