Skip to main content

#Najifunza 02; Huu ndio wakati sahihi wa kumjua vile mtu alivyo


Maisha ya Mwanadam yamejaa maigizo , na wengi wao hawapendi kuishi maisha yao(uhalisia wao). Na kwa namna hii huwezi kufahamu mtu kwa undani vile alivyo.Kwa sababu anaweza kuigiza maisha yasiyo yake na ukamwamini.

Lakini Wakati mzuri wa kumjua mtu vile alivyo ni pale anapopitia changamoto kubwa katika maisha yake. Hapo ndipo uhalisia wake huonekana, uimara wake, nguvu zake, akili zake na yote yanayomhusu 

Mwanafalsafa(Mstoa) aliwahi kusema maneno haya, 
" Difficulties are things that show a person what they are" __ Epictetus
Akiwa na maana hii kwamba,  magumu ni mambo ambayo yanamwonesha mtu jinsi alivyo.

Zinapofika nyakati ngumu , ndipo ambapo tunaweza kumjua mtu vizuri na hiki ndicho kipondi kizuri sana ambacho kinamwonesha mtu vile alivyo. Kwa sababu wakati wa Raha mtu anaweza kuigiza na akafanikiwa kufanya hivyo.

Ili kudhibitiisha uimara wako/kwamba umeimarika ni lazima magumu/changamoto uzipate ili kudhibitisha hilo.
Utawafahamu marafiki wa kweli pale ukikutana na magumu.
Utajua na kugundua uwezo wako na kukabiliana na changamoto, pale utakapozipata
Utajua uwezo wako wa kuzuia hisia ya Hasira pale ndugu, rafiki na mtu yeyote anapokuudhi
Hata kiongozi bora uwezo wake hujulikana pale magumu anapoyapata,  na sio wakati wa Amani .


Hatua ya Kuchukua; Unapopitia magumu, jitie nguvu na jiambie kuwa hayo ndiyo yanayokuonyesha vile ulivyo.
Hivyo pambana na hakikisha unashinda vyema  katika changamoto unayokutana nayo.

#Najifunza. 
_____________________________________
Makala hii imeandikwa na ; 
Joshua Golyama, ambaye ni Mwalimu, Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo, Mhamasishaji Wa Mafanikio na Mwandishi.



+255 764 257 495 / +255 622 163 323
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com
Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...