Skip to main content

AGRICULTURE 101; UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI


Habari rafiki mpendwa;

Ni matumaini yangu u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku , hongera kwa yote na endelea zaidi ili tuweze kufikia mafanikio makubwa zaidi

Karibu sana katika mtandao huu wa ELIMU KITAA(STREET EDUCATION) ambao unahusika na kutoa elimu kwa njia ya makala kuhusu mambo mbalimbali kama vile , Kilimo,  Afya,  ufugaji, Mafanikio binafsi , na makala zinazoelimisha zaidi kuhusu kulijua Kusudi la Mungu katika maisha yako, pia Mtandao huu unahusika pia kutoa makala zinazohusu Elimu ya Lishe na Matumizi ya Muda.

Lengo kuu la mtandao huu ni kushirikisha na kutoa maarifa sahihi kwa watu wote kuhusu maduala yote tunayokutana nayo katika maisha.
Huo ni utangulizi kiufupi kuhusu mtandao huu ,
Sasa nikukaribishe katika makala Ya AGRICULTURE 101 , ukurasa unaohusu masuala yot yanayohusu kilimo na mifugo,

Leo tunakwenda kujifunza kiufupi kuhusu ufugaji bora kwa Kuku wa Mayai .
Katika ufugaji wa aina mbili ambao unajulikana na kila mtu , ufugaji wa kuku wa mayai na ufugaji wa kuku wa nyama.
Tunakwenda kujifunza kiufupi, kuhusu kanuni za msingi za kuzingatia katika ufugaji wa Kuku wa Mayai na makal zijazo zitakuwa na maelezo ya kutosha zaidi kuhusu ufugaji wa kuku wa Mayai .

Kwanza kabisa , unachotakiwa kufahamu ni kuwa;Ili uweze kuwa na ufugaji bora  na wenye tija  zipo Kanuni chache za Kuzingatia, ambazo ni;

1.Kuchagua aina nzuri ya mnyama/ndege unayetaka kumfuga-Hii inategemea na mahitaji yako/malengo ya ufugaji , na mazingira uliyopo

2.Lishe bora.

3.Kutibu na kudhibiti Magonjwa

4 .Mazingira safi /mahali pa kuishi


Baada ya kujua Kanuni za Msingi katika ufugaji , Karibu tuendelee na Mafunzo yetu

Faida zinazopatikana kutokana na ufugaji wa kuku wa mayai

1. Huwapatia wafugaji lishe bora kwa kula baadhi ya mayai .

2.Huinua kipato cha kaya na familia kwa kuuza mayai ambayo hutagwa kwa wingi na kwa kila siku.

3. Hutoa ajira kwa watu wengi ambao huendesha shughuli zao kwa kufuga kuku wa mayai .

4. Humpatia mfugaji /mkulima mbolea ya kulimia na kukuzia mazao bustanini au shambani (kinuesi cha kuku).

5. Humpatia mfugaji fedha kutokana na mauzo ya mbolea , mauzo ya kuku ambao wameshakomaa kwa kutaga .

6. Humpatia mfugaji kitoweo kutokana na kuwachinja kuku waliokomaa kutaga .

7. Humpatia mkulima fedha kutokana na mauzo ya manyoya ya kuku waliochinjwa kwa ajili ya kutengeneza mito na mapambo .


KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA KISASA WA MAYAI .

1.Kwapa kuku malazi bora kwenye banda zuri

(a) Vifaranga 

_Andaa na safisha chumba cha kuwalelea , paa na kyta na sakafu

_ Tandaza pumba za mpunga au takataka za randa ambazo ni kavu na safi sakafuni

_Andaa mviringo wa kulelea vifaranga ili uwazuie wasizurure mbali na chanzo cha joto

_Ning'iniza balbu ya umeme au taa ya chemli ndani ya mviringo ili kuwapa vifaranga joto .

_Hakikisha banda lina hewa ya kutosha lakini haliingizi upepo mkali . Upepo na jua kali vinaweza kuvidhibiti kwa kuweka mapazia dirishani

(b) Kuku wakubwa .

_ Waandalie banda lenye sifa za vifaranga lakini usiwawekee mviringo wala chanzo cha joto.

_Wawekee vitundu au maboksi ya kutagia na majukwaaa ya kusimamia ya miti au mbao.

2. Kuchagua kampuni yenye vifaranga bora wa mayai 

Zipo kampuni nyingi ambazo ni maarufu kwa uuzaji wa vifaranga .Hata hivyo waone wafugaji maarufu na wafugaji wenye  wazoefu wa kufuga kuku wa mayai pamoja na wataalamu wa mifugo wa kuelekeze kwenye kampuni ambazo vinauza vifaranga bora.

3. Matunzo bora kwa kuwapa chakula bora , dawa , na maji wakati wote.

(a) Matunzo kwa vifaranga

_Andaa chakula cha vifaranga

_Andaa maji safi na salama

_Safisha vyombo vya kulishia na kunywesha

_Andaa dawa ya kudhibiti magonjwa na vimelea

_Weka mviringo ndani ya banda , vyombo vya kulishia na kunyweshea ndani ya mviringo .

_Washa taa au balbu iliyoning'inizwa katikati ya mviringo.

_Weka maji kwenye chombo cha maji na chakula kwenye chombo cha chakula

_Watoe vifaranga kwenye maboksi uwainginize ndani ya mviringo

_Wapatie chakula cha kutosha mara mbili kwa siku
_Wapatie maji safi na salama ya kutosha mara mbili kwa siku .

_Hakikisha hoto halipungui kwenye 32c na halizidi 35c  Pandisha balbu juu kupunguza joto au shusha balbu ili kuongeza joto.

_Panua mviringo Kulingana na kasi ya kukua kwa vifaranga wako, Wanapitimiza mwezi mmoja .

_Usisahau kuweka kumbukumbu ya :-
        Tarehe na idadi ya vufaranga vilivyonunuliwa
        Idadi ya vifo, tarehe na sababu ya vifo vyao
        Idadi ya waliopo
        Kama ulitokea ugonjwa , andika  dawa iliyowaponya
        Kiasi cha chakula unachowalisha kila siku

(b) Matunzo kwa kuku wanaokua.

_Jinsi kuku wanvyoendelea kukua ndivyo wabavyopunguza ulaji wa chakula .Wape kuku wa mwezi mmoja hadi minne chakula cha kukuza kama kama kilo 28 kwa siku kwa kuku 100.Wape maji safi na salama ya kutosha

_Wape kuku wanaotaga chakula cha kutosha yaani kilo 15 hadi 18 kwa siku kwa kuku 100..Wapatie maji safi na salama ya kutosha na ikiwezekana wapatie vitamini na madini maalumj kwa ajili ya kuku.

4. Usafi wa vyombo vya chakula na maji
Vyombo hivi vinatakiwa vitunzwe katika hali ya usafi .Kinyume cha hivyo huweza kuwa ni chanzo kikuu cha Magonjwa mbalimbali.

(i)Hakikisha chombo cha kunyweshea maji hakivuji ili kisije kikalowanisha pumba na sakafu.

(ii)Hakikisha chombo cha chakula nacho hakijatoboka popote ili kisije mwaga chakula hasa kwa vile vinavyotundikwa .

(iii) Wakati wa kuwawekea kuku chakula , na maji , mwaga mabaki  kisha safisha na kukausha vyombo ndipo uweke chakula na maji.

(iv) Ni vyema uwe na vyombo zaidi ya seti moja ili viweze kutumika wakati vingine vikikauka juani.

5. Usafi wa banda na mazingira ya ndani ya banda. Tahadhali za hali ya juu zisipo chukuliwa kulinda usafi katika banda,  kuku wanaweza wakapata matatizo ya kyshikwa na Magonjwa mbalimbali.Hivyo basi;

(1) Hakikisha banda halina vumbi na tando za buibui kwa wingi

(2) Hakikisha Pumba au takataka za randa ulizotandaza sakafuni hazilowi na maji na kama zikimwagikiwa na maji kwa bahati mbaya, ziondolewe na kuwekwa pumba nyingine kavu na safi


(3) Pumba zikishakaa kwa muda mrefu bandani hulowanishwa na vinyesi vya kuku, na huchafua miguu ya kuku .Hivyo basi hakikisha  unabadilisha pumba kabla hazijalowana sana .

Makala hii itaendelea....



Makala hii imeandikwa na; 
Joshua Golyama 
Mwanafunzi wa Shahada Ya Awali ya Sayansi Ya Kilimo 
Chuo Kikuu cha Sokoin Cha Kilimo (SUA-MOROGORO)
+255764257495/0622163323
Baruapepe;golyamajoshua@gmail.com
Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...