Skip to main content

KURASA 01; Hiki ndicho kinachokukwamisha usipate mafanikio.


Habari  yako  mpendwa,
Natumai  u  mzima  na  unaendelea  na  majukumu yako  ya  kila  siku.
Karibu  sana  tuweze  kujifunza  na  kupata  maarifa  ili  tuweze  kuwa  bora  zaidi  na  kuwa  na mafanikio  makubwa   katika  maisha  yetu .

Hakuna  mtu  hata  mmoja  ambaye  anapenda kushindwa,  kila  mtu  anatamani  afanye  vizuri na apate  mafanikio  makubwa  sana.
Hakuna  mtu  anayependa  kuwa  masikini,  kila mtu  anapenda  awe  tajiri  na  kufanikiwa  katika kila  jambo  analolipanga  kulifikia.
Kila  mmoja  anapenda  kufikia  viwango  vya  juu sana  vya  mafanikio,  na  hata  wanafunzi  shuleni hakuna  anayetamani  kufeli katika  mitihani  yake.

Na  ukweli  ni  kwamba  yule  aliye  tajiri  na masikini  wote  ni  binadamu,  na  wote  tupo duniani tuna masaa yale yale 24 na  wana  kila  kitu ambavyo  hata  wewe  unacho.

Kipo  kitu  kimoja  tu  ambacho  hutofautisha  kati ya  Masikini  na  Tajiri, wasiofanikiwa  na  wale  waliofanikiwa.
Kitu  hicho  ni  MTAZAMO(attitude)  juu  ya  maisha yao.
Kinachowafanya  waliofanikiwa  kufanikiwa ni kuwa  wana  mitazamo  chanya  ambayo inawasukuma  na  kuwasaidia  kufikia  hapo  wanapofikia.
Ili  uweze  kufanikiwa  katika  kila  jambo unalolifanya,  unatakiwa  kuwa  na  mtazamo chanya,  juu  ya  kile  unachokitaka.
Haijalishi  una  ndoto  kubwa  kiasi  gani,  au mipango  na  malengo  mengi  kiasi  gani,  ila usipokuwa  na  mtazamo  chanya  hauwezi  kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako.

Wapo  watu  ambao  wanatamani  kufanya makubwa  katika  maisha  yao,  Lakini  hawana Imani  kuwa  wanaweza  kufikia  mafanikio hayo.
Mtu  anatamani  kuwa  tajiri  lakini  hana   mtazamo  chanya  wa  kuwa  Tajiri.
Lazima  uubadili  mtazamo  wako  ili  uweze  kufanikiwa

Kuwa  na  mitazamo  hasi  hakuwezi  kukusaidia kufikia  mafanikio  makubwa.
Mtazamo  ni  ile  picha  ya  ndani  unayoiona  juu ya  kile  unachokipanga  katika  maisha  yako.
Kuona  kwamba  unaweza  kufikia  mafaniko  makubwa.
Kuona  kwamba  unaweza  kuwa  tajiri .
Kuona  kwamba  ndani  yako  una  nguvu isiyopimika  ya   kukusaidia   kufanya  mambo makubwa   sana  katika  maisha  yako.

Licha  ya  kuweka  malengo  na  kuwa  na  ndoto kubwa ,  unapaswa  pia  kuyaamini  malengo  na ndoto  zako  kwamba  unaweza  kuzifikia.
Jiamini  wewe  mwenyewe  binafsi  na  kuona kwamba  unaweza  kufikia  mafanikio  makubwa.

Badili  mtazamo  wako  juu  ya  maisha  yako,  Jione mtu  uliyefanikiwa  tayari  na  kuona  pia umeshamiliki  kiwango  cha  pesa  unachokihitaji katika  maisha  yako.
Jione  kuwa  wewe   unaweza  na  hakuna  linaloweza kukukwamisha  kufikia  mafanikio yako.
Uwe  na  imani  kuwa   utafikia  ndoto  zile  ulizo nazo.

Hiki  ndicho  kinachokukwamisha  wewe usifanikiwe,  hujiamini  wewe  mwenyewe  na kuamini  pia  kwamba  utafikia  malengo uliyojiwekea.
Vile  unavojiona  kuhusiana  na  malengo  yako,  na namna  unavyoyachukulia  malengo yako,  ndiko kunakoweza  kukusaidia  kutambua  kama  utaweza  kufika  au  la!
Jiamini  wewe  mwenyewe,  tengeneza  picha  halisi ya  kule  unakotaka  kufika,  Yaani  uone mwanzoni vile  utakavyokuwa  hapo  baadaye.
Fanya  kwa  namna  ya  kuona  kama  umeshafikia malengo  yako.

Hatua ya Kuchukua;

Kitambue  kile  unachokitaka  katika  maisha  yako, uwe  na  ndoto  kubwa  na  malengo  makubwa   katika  hilo, na  Amini  kuwa  Unaweza  kufikia mafanikio  na malengo  hayo  uliyojiwekea

Tafakari  na  uelewe  ni  kiwango  kipi  cha  mafanikio  unakihitaji  katika  maisha  yako,  utajiri,  fedha,  afya,  masomo n.k.
Weka  picha  halisi  moyoni  mwako  na  kuona  kule  mbele  unakokutaka.
Uone  mwisho  wako ,  mwanzoni


Kama  unahitaji  kuwa  Billionea,  ona  unamiliki fedha  hizo  tayari,  yaani  kile  unachokihitaji  kione tayari  unacho.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...