Skip to main content

TUMIA MUDA WAKO VIZURI, CHAGUA MAMBO MACHACHE NA UYAFANYE HAYO

Habari ya kwako rafiki na ndugu yangu Mpendwa,
Natumai u mzima na unaendelea vyema na majukumu ya Kila siku , nikukaribishe sana katika Makala hii ili tuweze kujifunza na kuweza kuwa bora katika maisha yetu.
Tunatakiwa kufanya kazi, na vyote tuvifanyavyo kwa bidii , lakini sio kwa bidii tu bali KATIKA UBORA .

Makala hii inaeleza namna gani tunavyoweza kutumia muda wetu vizuri,
Watu wengi hulalamika sana na wakati mwingine kuwalaumu watu wengine kwamba wanawapotezea Muda wao, lakini kumbe hawajajua , hutakiwi kumlaumu mtu yeyote, anza wewe mwenyewe
Wewe ndio chanzo kikubwa sana cha kupoteza muda

Mpendwa upo msemo unaosema "mambo mengi muda muchache" msemo huu umekuwa maarufu sana , na wakati mwingine umekuwa unatumika kama sababu ya kuitumia pale anapoona anashindwa kuyafanya yale anayotamani kuyafanya .Muda upo mwingi sana , na ukweli ni kwamba "hakuna muda wa kutosha kufanya kila kitu , ila upo muda wa kutosha sana kufanya yale ya muhimu zaidi.
Hivyo karibu tujifunze kwa Pamoja tujue nini tunatakiwa kukifanya.

Jifunze, na yachukue ukayatendee kazi yatakusaidia sana.
Karibu Tujifunze pamoja;

Nguvu, Muda na Juhudi Unayoitumia Kuyasema na Kuyachambua Maisha Ya watu wengine
Kuwakosoa kwa Yale wanayoyafanya , NI VEMA SANA ukahamisha Nguvu hizo , Muda huo na Juhudi katika UWEKEZAJI BINAFSI wa Mtazamo wako na KUKUA ZAIDI na Kufikiria Zaidi Maisha Yako na Namna Utakavyoweza Kufanikiwa.

Wekeza Zaidi Katika KUJIFUNZA , bila Kujifunza Huwezi kupata MAFANIKIO .
Pake tu utakapoacha Kujifunza , ndipo unaingia Hatarini zaidi Ya Kuangamia Katika Maisha Yako .
Unaweza Kujifunza KUTOKA KWA WALE WALIOFANIKIWA ZAIDI YAKO katika Maisha .
Maana Wana Kitu cha Kukufundisha Na Kukupa Mwanga Kule unakotamani Kufika .

Wekeza NGUVU ZAKO, MUDA WAKO NA JUHUDI KUBWA kutafuta MAARIFA ya Kile Ulichobobea,  Yawezekana Kazi unayoifanya , au Biashara n.k.
Tafuta Maarifa zaidi ili uweze Kuwa Bora na Kazi au Shughuli  unayoifanya  kuwa Bora zaidi .
         Unaweza Kupata Maarifa na Kujifunza Kwa Kufanya Yafuatayo:-

1.Kusoma Vitabu; Vitabu vyenye Mafundisho Ya Msingi na Vinavyoweza Kukusaidia Kupata Maarifa Unayitamani Kuyapata .
Hapa Simaanishi Vitabu Vya Hadithi ,  bali vitabu vyenye maelekezo au Kanuni Fulani kuhusu Jambo Fulani .Unaweza pia Kuvitafuta  Vitabu Vinavyohusu  fani Yako au Kazi Unayofanya ,  Mfano Kilimo,  Ufugaji Na kazi Nyinginezo ambazo unaweza Kufanya .

2.Kuhudhuria Semina Mbalimbali Zinazotoa Elimu kuhusu Fani au Kazi Yako ,  Mfano Semina za Ujasiriamali , Mifugo Kilimo n.k.
Hizi zinakufanya Kupata Maarifa Ambayo Yanaweza Kukusaidia Kwa Bora zaidi na Kukua Zaidi .
Lakini pia katika Semina Unapata Nafasi ya Kukutana na Watu Mbalimbali ambao Wanaweza Kukuhamasisha Kusonga na Pengine kukueleza Uzoefu walio nao Juu ya Jambo Fulani .

3 .Kusikiliza CD,  TAPE na Sauti (AUDIOS )Pia Redioni ,  na Kufuatilia Na Kutafuta Maarifa Kwenye Mitandao ya Kijamii pamoja Na Televisheni
Katika Maeneo hayo unaweza Kujifunza na Kukupa maarifa yanayoweza kukufanya kuwa bora sana .

Tumia MUDA WAKO MWINGI katika Mambo machache na Ya MUHIMU katika Maisha Yako.
Na Sio kutumia Muda Wako katika Mambo Yasiyo na Msaada Katika Maisha Yako .

KUMBUKA; Watu wengi wanashindwa Kufanikiwa na Kuweza Kutimiza Malengo yao ,  ni KWA SABABU YA KUFANYA MAMBO AMBAYO HAYANA MCGANGO WOWOTE KATIKA KUFIKIA MALENGO YAO .
Kama unafanya Mambo ambayo hayana Mchango wowote Katika Maisha Yako ACHANA NAYO ,
kwa sababu Yanakupotezea Muda Sana na Kukufanya kutofikia Malengo Yako .


WEKEZA MUDA WAKO KATIKA kulitafuta KUSUDI LA MUNGU katika Maisha Yako.

Maana Ya KUSUDI; Kusudi ni Sababu Ya asili ya Kuwepo (kuumbwa ) kwa kitu fulani.
Kusudi ni sababu ya kuwepo kwa kitu fulani au sababu ya Kufanyika kwa jambo fulani.

Swali la KUJIULIZA ; Mimi ni nani? , Mimi nipo duniani kwa Kusudi gani?
  Kitu chochote kipo kwa Kusudi Maalumu.
  Kila jambo linalofanyika chini ya jua hufanyika kwa kusudi maalumu.
  Katika kitu chochote kilichoumbwa  kuna sababu ya Asili iliyosababisha kuumbwa kwa kitu hicho.

JIFUNZE MAMBO YAFUATAYO SIKU YA LEO.
  Kusudi La Mungu ni Msingi pekee wa Uumbaji wa Mungu .
Mungu ndiye Mwanzilishi wa Kusudi la kila kitu.Ipo Sababu ya kubwa sana ya Mungu kuumba dunia na Vyote vilivyomo nayo ni KUUDHIHIRISHA UKUU WAKE kupitia UUMBAJI

Waefeso 1:11 ".... na ndani yake sisi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali , sawasawa na KUSUDI LAKE Yeye ambaye hufanya mambo yote kwa Shauri la Mapenzi yake"
 
    Pasipo KUSUDI maisha Hupoteza Maana.
Hata kama mtu akawa na Mali nyingi , watoto wengi   
asipolitambua Kusudi lake la Kuwepo duniani , maisha Yake hayatakuwa na Maana Kabisa
" Kusudi huamua maisha , hakuna maisha pasipo Kusudi "

      Uliumbwa Kwa "KUSUDI MAALUMU" ili kukamilisha "KUSUDI KUU"
Kusudi maalumu(Kusudi Binafsi) - Uwepo wako ni udhihirisho kuwa kuna jambo kubwa , lililoamua uwepo wako hapa Duniani "Kusudi Binafsi"
Upo duniani kwa kuwa lipo jambo ambalo haliwezi kukamlishwa na mtu Mwingine yeyote isipokuwa WEWE.
Kila Mtu aliumbwa kwa Kusudi ambalo yeye tu ndiye aliyepewa MAMLAKA (UWEZO ) wa Kulikamilisha .
Kusudi kuu - Kusudi kuu la Uumbaji Wa Mungu ni KUTAKA MWANADAMU AWE MTAWALA WA UUMBAJI WAKE
Utawala wa Uumbaji wa Mungu utakamilishwa Tu pale utakapolifahamu Kusudi Binafsi(Kusudi Maalumu)

Kusudi Lako Ndilo liliobeba Mamlaka Yako Ya KUTAWALA katika ULIMWENGU HUU.

   Thamani Ya Mtu yeyote duniani imefichwa katika uwezo wako wa KUTAMBUA Wewe ni Nani? Na uliumbwa Kufanya nini hapa Duniani
Kutolijua Kusudi La Mungu Katika Maisha Yako ni Sawa na Kuamua KUCHAGUA kupoteza Thamani Yako hapa Duniani..

Najua umejifunza kitu kutoka katika Makala hii,
Chukua na nenda kayatendew kazi yatakusaidia na kuongeza hatua mbele zaidi katika maisha yako
Mungu akubariki sana
Ahsante.

Makala hii imeandikwa na ;
Joshua Golyama
Mwanafunzi wa Shahada Ya Awali  ya Sayansi ya Kilimo
Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo(SUA-MOROGORO)
+255764257495
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com
Blogu;elimukitaa2020.blogspot.com.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...