Skip to main content

Posts

MAKALA 01; RAFIKI BORA NI VITABU (THE BEST FRIEND IS BOOKS)

  MAKALA 01; RAFIKI BORA NI VITABU (THE BEST FRIEND IS BOOKS)   Habari yako rafiki yangu, Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya kabisa, Karibu katika mfulululizo wa makala hizi kutoka katika kitengo cha KUTOKA VITABUNI, Ili kuweza kuwa bora katika maisha yako ni vyema sana ukaambatana na kuzungukwa na watu walio na kile ambacho wewe unataka kuwa. Ni asilimia 85% ya mafanikio yako huchangiwa na watu wanaokuzunguka.   Marafiki zako, ndugu zako na jamaa zako ambao unatumia muda mwingi kuwa nao kazini, shuleni, ofisini na maeneo mbalimbali ni muhimu wakachunguzwa na kuona kama wanaweza kukupeleka kule ambako unataka kufika. Upo msemo wa Kiswahili ambao huzungumzwa kwamba ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi, hii humaanisha kwamba ukiambatana na mtu mwenye tabia Fulani,automatically kuna baadhi ya mambo ambayo utayavuta kutoka kwa rafiki yako. Eneo hili ni muhimu sana kwa sababu linachangia kwa kiwango kikubwa katika mafanikio yetu na katika safari ya kufika ku...

MY MEMORIES _MY BRAIN REMEMBER THIS

  MY MEMORIES _MY BRAIN REMEMBER THIS . Wakati nikiwa mdogo sana, nilijiona nikiwa mwalimu mkubwa sana na mwenye maisha fulani mazuri. Wakati mwingine nilikuwa na ndoto za kuwa daktari bingwa (Specialization). Ambapo kwa mara ya kwanza nilitamani sana kuwa Daktari aliyebobea kwenye masuala ya kutibu meno. Nikiwa naanza Kidato cha kwanza, wazo la ualimu liliendelea kuishi ndani yangu hadi kidato cha tatu, ambapo nilibadili wazo hilo na kuanza kufikiri kuwa Mhandishi wa Barabara (Civil Engineering) na nikaanza kuongeza juhudi kabisa katika Hesabu ili niweze kufanya vizuri katika hesabu na kupata nafasi ya kwenda kusomea Mchepuo wa PCM. Na ninachokumbuka ni kwamba katika mawazo yote hayo niliyokuwa na ndoto nilizokuwa nazo, nilipenda sana kuwaelekeza wengine pale ambapo hawaelewi na wakati mwingine kujipendekeza kuelekeza hata kama sijaombwa kufanya hivyo. Lakini baadaye kidogo (Mwishoni mwa Kidato cha nne), Nikawaza kuwa Daktari wa Masikio na wazo hili alilirudia mama yangu, baada ya...

ANZA SASA, UMRI USIWE KIKWAZO CHA WEWE KUTOTIMIZA NDOTO ZAKO

 ANZA SASA KUFANYA, UMRI ISIWE KIKWAZO KWAKO. Bila shaka unayo maono fulani (Unajiona ukiwa unafanya kitu baadaye ambacho ni kikubwa sana). Kwa namna fulani unatambua jambo fulani unaweza kulifanya kwa ufanisi mkubwa kabisa. Na unajua kabisa, kwamba utakapofanya jambo lile utakuwa katika viwango fulani vikubwa sana. Lakini, mbona huanzi? Nini kinakukwamisha usiendelee?  Ni ujuzi, Maarifa, huelewi pa kuanzia? Au unasema ngoja nikue kidogo au nifikie hatua fulani?. Tuko watu ambao tunasubiri hadi tufike viwango fulani vya Elimu ndipo tuanze kutumiza ndoto zetu. Tuko watu tunaosubiri tufikie Umri fulani ili tuanze kutimiza ndoto zetu. Lakini tunajichelewesha wenyewe, umri sio tatizo kabisa. Kwani haujaona Watu wakiwa na Umri mdogo na wanafanya Makubwa?. Je, Mastaa wengi katika tasnina mbalimbali duniani wana Miaka mingapi hadi muda huu na walianza wakiwa na Miaka mingapi? Je, Mabilionea wa Dunia wana Miaka mingapi muda huu?. Je unamfahamu Rev Victor Githu  kutoka Kenya ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...

JENGA TABIA YA KUJIFUNZA KILA WAKATI , ONDOA KIBURI KATIKA KUJIFUNZA.

JENGA TABIA YA KUJIFUNZA KILA WAKATI ,  ONDOA KIBURI KATIKA KUJIFUNZA. Unapokosa tabia ya kujifunza na kuwa na hali ya kujiona unajua kila kitu utakuwa nayo na Kwa Maana Hiyo hautaweza kuwa na spirit ya kuendelea kujifunza zaidi na zaidi. Lakini unapokuwa unajifunza kila wakati, utagundua kwamba Mambo mengi huyajui hii itaamusha Nguvu mpya, ari mpya na hamasa ya kue ndelea kujifunza zaidi. Jifunze zaidi ili upate hamasa ya kujifunza zaidi. Na MUHIMU,  ili uweze kujifunza ni lazima ujione hujui , na kama utaona kama unajua kamwe hautaweza kujifunza Kwa maneno Mengine unakuwa na KIBURI KATIKA KUJIFUNZA ambacho Kinakuzuia wewe kujifunza zaidi, kwa sababu ndani yako kutakuwa na Sauti kama hii  'mbona kila kitu ninakijua, kujifunza ni kupoteza muda' Hakikisha unajitahidi unakuwa na Tabia Ya KUJIFUNZA, kwa sababu katika Karne hii Ya 21 kuna Maendeleo makubwa sana Ya Teknolojia na Ni ULIMWENGU WA TAARIFA hivyo usipojifunza kamwe hauwezi kuwa na Taarifa sa...

HEKIMA YA SIKU; Kila Jambo ulifanyalo lifanye kama wajibu na si kutegemea shukrani au kutambulika

Kila jambo unalolifanya, lifanye kama wajibu, na usifanye ukitegemea kutambuliwa, au kupewa shukrani. Watu wengi  wanapata shida sana  pale ambapo wanafanya mambo mengi, na hakuna anayeonekana kuwashukuru kwa yale wanayoyafanya. Unajitoa kwa nguvu zako kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa. Fuatilia mifano hii michache ili uweze kupata kile ninachokimaanisha hapa; Mfano  wa kwanza; Viongozi mbalimbali tulio nao, wanatumia muda wao mwingi na nguvu nyingi kuhakikisha wale wanaowaongoza wanafika pale wanapotakiwa kuwa. Na  hakuna hata mmoja anayetambua mchango wao na nguvu zao walizotumia kuwaongoza. Na pengine asiwepo hata mmoja wa kusema asante kwa yale wanayafanya. Mfano wa Pili ; kwenye mahusiano,unakuta boyfriend/girlfriend anafanya kila anachoweza ili kuboresha mahusiano yao, kumsaidia kwa kila hali/changamoto anayoipitia Lakini haoni mwenzie akimshukuru au kutambua kwa kile anakifanya. Mfano wa tatu; Kazini kwako, unafanya kila kitu vile inavyotaki...

KUWA MAKINI SANA NA NAMNA UNAVYOTUMIA MUDA WAKO

KUWA MAKINI SANA NA NAMNA UNAVYOTUMIA MUDA WAKO "Muda ni wa thamani sana kuliko fedha , unaweza kuzipata fedha kila siku Lakini muda hauwezi kuupata ukishaupoteza. Hivyo, tunatakiwa muda vizuri ule tunaoupata na kwa umakini mkubwa zaidi. Epuka kupoteza muda kwa kutofanya yale yasiyo na umuhimu kwako. Maana wengi tunahangaika na mambo mengi sana ambayo hayana mchangi wowote katika maisha yetu. Pale upatapo nafasi ya kufanya jambo, hakikisha unalikamilisha na kwa usahihi kabla ya kuanza kufanya jambo jingine. Wekeza muda wako kwa kujifunza zaidi , wekeza zaidi ndani yako, ilishe akili yako maarifa mapya kila siku ili kuweza kuwa na mabadiliko makubwa hapo baadaye. Wekeza ndani yako kwa kusoma vitabu, kusoma Makala na kuhudhuria semina mbalimbali Jifunze kila siku na hii ni ni namna sahihi ya kutumia muda wako Vizuri. Huwa napenda kusema kuwa, watu wengi tunalalamika na kukiri kwamba " muda mchache , na Mambo mengi, Swali langu ni hili Je,  hayo Mengi uliyo nayo...