MY MEMORIES _MY BRAIN REMEMBER THIS.
Wakati nikiwa mdogo sana, nilijiona nikiwa mwalimu mkubwa sana na mwenye maisha fulani mazuri.
Wakati mwingine nilikuwa na ndoto za kuwa daktari bingwa (Specialization). Ambapo kwa mara ya kwanza nilitamani sana kuwa Daktari aliyebobea kwenye masuala ya kutibu meno.
Nikiwa naanza Kidato cha kwanza, wazo la ualimu liliendelea kuishi ndani yangu hadi kidato cha tatu, ambapo nilibadili wazo hilo na kuanza kufikiri kuwa Mhandishi wa Barabara (Civil Engineering) na nikaanza kuongeza juhudi kabisa katika Hesabu ili niweze kufanya vizuri katika hesabu na kupata nafasi ya kwenda kusomea Mchepuo wa PCM.
Na ninachokumbuka ni kwamba katika mawazo yote hayo niliyokuwa na ndoto nilizokuwa nazo, nilipenda sana kuwaelekeza wengine pale ambapo hawaelewi na wakati mwingine kujipendekeza kuelekeza hata kama sijaombwa kufanya hivyo.
Lakini baadaye kidogo (Mwishoni mwa Kidato cha nne), Nikawaza kuwa Daktari wa Masikio na wazo hili alilirudia mama yangu, baada ya mimi kumuuliza swali "Ety mama unataka niwe Daktari wa nini?" Na Mama yangu akanijibu kuwa anapenda niwe Daktari wa Masikio.
Na Kumbukumbu yangu inaniambia kwamba;Baada ya kuhitimu masomo yangu ya kidato cha nne. Nilianza kutumia simu na kwa mara ya kwanza nilifungua akaunti yangu katika moja ya mtandao wa kijamii (Facebook) na nikafungua pia Ukurasa wa Facebook ulioitwa 'fanatic general' na baadaye 'Ukurasa mwingine ulioitwa "Maneno Ya Ushindi". Katika akaunti hiyo na kurasa zake nilikuwa napenda sana kupakia maandishi yangu huko kila siku na kila wakati nikipata nafasi ya kufanya hivyo. Haijalishi nina cha kuandika au sina lakini nilihakikisha nimeandikia chochote katika kurasa hizo.........
Nilipata neema ya kufaulu mtihani wangu wa Kidato cha nne na Kujiunga na Kidato cha Tano, mchepuo wa PCB katika moja ya shule kubwa pale Mkoani Njombe. Huku nikijiona kabisa nikiwa daktari.
Nisingependa kuendelea sana na historia hii Fupi ya Maisha yangu.
Ninachoweza kusema ni kwamba "Hadi muda huu ndoto ya kuwa daktari haipo kabisa ndani yangu"
Ninachotaka kusema ni Hiki;
Mwaka 2018 nilipokuwa najiunga na Chuo Kikuu, ndipo nilipoanza kusoma Vitabu. Na Kitabu cha kwanza kukisoma kilikuwa ni kinaitwa CHANGING YOUR THINKING CHANGING YOUR LIFE kilichoandikwa na Brian Tracy, kItabu hiki kilinibadilisha sana namna ya kuwaza na kuwa na mtazamo tofauti kabisa na vile nilivyokuwa kabla.
Na kitabu cha Pili kilikuwa ni Who am I? Why Am I here? cha Sunday Adelaja. Kitabu kilinisaidia sana kujijua mimi ni nani na nimeumba kufanya nini hapa duniani.
Kilinisaidia kujijua ni mambo gani ambayo nayaweza zaidi kuliko mengine.
BAADA YA MAELEZO HAYO MAFUPI , Ninayo mambo Machache Muhimu nataka kukushirikisha leo;
PENDA NA JENGA TABIA YA KUSOMA VITABU.
Vitabu vinakufungulia dunia vile ilivyo. Inakupa maarifa sahihi.
Ndugu yangu iko watu wengi huishi maisha ambayo hawayafurahii kabisa, na kuona kama hana sababu ya kuendelea kuwepo duniani.
Ziko ndoto nyingi sana ambazo watu walikuwa nazo wakiwa wadogo lakini sasa zimepotea, sababu kubwa Hasa Ni KUKOSA MAARIFA sahihi yenye kuwasaidia Kujua KUSUDI LAO HAPA duniani n namna gani wanaweza kutimiza ndoto zao.
Watu wengi tupo gizani bado, Akili zetu na bongo zetu bado hazijapata nuru (bado hazioni kitu). Hatujajua ni mahali gani ambapo tunaweza kupata Nuru ambayo itatuangazia FIKRA ZETU zilizo gizani bado.
Leo nataka kukushirikisha jambo hili kuwa TUNAWEZA KUPATA MAARIFA kwa Kupitia KUSOMA VITABU. Mambo mengi ambayo huyafahamu utaweza kuyafahamu hayo baada ya kusoma Vitabu.
VITABU vinatupa UFAHAMU ( kwa yale tusiyoyafahamu bado) na Kisha Kupata MAARIFA kutoka kwenye UFAHAMU na baada ya kutumia MAARIFA tuliyo yapokea na kuyapata kwa usahihi tunakuwa ni watu wenye hekima.
Hivyo nikuhamasishe zaidi na zaidi uweze kujenga tabia ya kusoma vitabu ili uwezw kufumbuliwa macho.
Changamoto na yale yote unayodhani hayawezi kufanyika, Yanawezekana baada ya KUANZA KUSOMA VITABU kwa kuwa vitakupa mtazamo mpya wa namna ya kuyaendea mambo mbalimbali katika maisha.
Najua umenielewa. Nayawezwekana hadi muda huu hujajua Kitabu cha Kusoma.
Nikushauri sasa Kukipata kitabu Hiki Cha SIJAANZA KUISHI kilichoandikwa na Mwanadada Winnie Simplis.
Kwanini SIJAANZA KUISHI.
Ninakushauri kukisoma kitabu hiki kwa sababu zifuatazo;
1. Kinatoa na kukupa mwanga wa Kwanini mpaka sasa umeshindwa kumwona yule mtu uliyekuwa unamwon ukiwa mdogo.
2. Kinakusaidia kujua Uwezo wa Kipekee ambao Mungu ameweka ndani yako.
3. Kitakusaidia kujijua na kutambua KUSUDI LA MUNGU katika maisha yako.
4.Kitakuonyesha kama kweli umeanza kuishi au la?
Inawezekana upo ila bado haujaanza kuishi, Najua nimekuchanganya hapa na pengine kushindwa Kuelewa. Ukikisoma kitabu hiki kitakusaidia kujibu maswali hayo ambayo unajiuliza. Mimi sikuyajua kabla. Ila baada ya kusoma Kitabu kile nimeweza kujua kama ninaishi au bado Sijaanza.
Bila shaka umepata shauku ya kuanza kusoma vitabu sasa. Wasiliana na mimi ili nikupe maelekezo ya namna ya kuchagua vitabu vya kusoma na Namna ya kuvisoma.
Pia, Kama unahitaji Kupata Nakala Yako ya Kitabu hiki cha SIJAANZA KUISHI. Wasiliana nami nikupe maelekezo ya Kukipata nakala yako.
Au tumia mawasiliano yaliyopo hapa chini kwenye Picha ili nakala yako kwa mkoa wowote uliopo hapa TANZANIA.
Sijaanza Kuishi Na Winnie Simplis.
See You Shining And Enjoying The Cake!
Joshua Golyama
(Author | Motivational Speaker | Teacher | Blogget).
+255 764 257 495 (Whatsapp).
golyamajoshua@gmail.com
elimukitaa2020.blogspot.com
"I se The Whole World Enjoying Because Of Me"
Comments
Post a Comment