Skip to main content

MAKALA 01; RAFIKI BORA NI VITABU (THE BEST FRIEND IS BOOKS)

 MAKALA 01; RAFIKI BORA NI VITABU (THE BEST FRIEND IS BOOKS)

 Habari yako rafiki yangu, Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya kabisa,

Karibu katika mfulululizo wa makala hizi kutoka katika kitengo cha KUTOKA VITABUNI,

Ili kuweza kuwa bora katika maisha yako ni vyema sana ukaambatana na kuzungukwa na watu walio na kile ambacho wewe unataka kuwa. Ni asilimia 85% ya mafanikio yako huchangiwa na watu wanaokuzunguka.  

Marafiki zako, ndugu zako na jamaa zako ambao unatumia muda mwingi kuwa nao kazini, shuleni, ofisini na maeneo mbalimbali ni muhimu wakachunguzwa na kuona kama wanaweza kukupeleka kule ambako unataka kufika.

Upo msemo wa Kiswahili ambao huzungumzwa kwamba ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi, hii humaanisha kwamba ukiambatana na mtu mwenye tabia Fulani,automatically kuna baadhi ya mambo ambayo utayavuta kutoka kwa rafiki yako.

Eneo hili ni muhimu sana kwa sababu linachangia kwa kiwango kikubwa katika mafanikio yetu na katika safari ya kufika kule ambako tunatamani kufika.

Neno la Mungu linadhibitisha hili; Tuangalie mifano michache hapa;

Mithali 13:20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima. Bali rafiki wa wapumbavu ataumia

Mithali 22:24-25 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; wala usiende  na mtu  wa ghadhabu nyingi;

Usije ukajifunza njia  zake; na kujipatia nafsi yako mtego.

Mithalio 27:19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake”

Mithali 27:17 “Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu auonoavyo uso wa rafiki yake”

Kutoka kwenye mifano michache ambayo tumeiona hapo juu tunajifunza mambo ambayo hutokea pale tunapokuwa tunaambatana na wale marafiki zetu, familia na wengine na matokeo yake.

Mfalme Sulemani anatufundisha hapa kwamba Kamwe usifanye urafiki na   mtu mwenye hasira kwa sababu unaweza kujifunza pia na wewe.

Unapokuwa unatumia muda wako mwingi na rafiki yako, kuna kuambukizana tabia kunatokea. Hivyo kuna baadhi ya mambo mtaanza kufanana katika mitazamo na hata utendaji wake.

Tunajifunza pia kwamba ili kuwa mtu mwenye hekima ni lazima uambatane na wenye hekima, utumie muda wako mwingi na watu wa aina hiyo.

Najua unayo ndoto ambayo unatamani kuitimiza katika maisha yako, jambo  la muhimu sana ambalo unatakiwa kuwa nalo makini ni AINA YA MARAFIKI utakaoambatana nao. Bila shaka utapaswa kuwa makini hasa kuchunguza mitazamo waliyo nayo, na hata ndoto zao, misimamo yao na kuona kama inafanana na wewe na kukusaidia kukuvusha sehemu moja kwenda nyingine katika safari ya mafanikio yako.

Moja ya marafiki ambao unaweza kuwachagua kuambatana nao na ukatumia muda wako mwingi ni VITABU. Najua unashangaa hapa kidogo lakini ambatana na mimi katika kusoma makala hii utajifunza na kujua hasa  kwanini kuambatana na VITABU.

Waliotutangulia walijihusisha katika mambo mengi sana, kuna mahali walifana vizuri sana, kuna mahali walifanya vibaya na hayo yote wameyandika kwenye VITABU. Naweza kusema kuwa Kitabu ni moja ya hazina kubwa sana ambayo wazee wetu wa zamani walituachia, na hata sisi tunawaachia na tutawaachia yale tunayoendelea kujifunza kila siku.

Kwenye vitabu kuna kila kitu ambacho wewe unakihitaji ili kufikia ndoto zako kwa mafanikio makubwa sana. Unapata kuhamasika na yale ambayo yalifanyika hapo zamani yanayofanana na lile ambalo wewe unalifanya.

In the books you extract the positive mindset that is needed in accomplishing your dreams/purpose and enables you to live victorious life.

Unatakiwa kuambatana na Yule ambaye haamini katika kushindwa na badala yake anaamini katika kushinda. Mwenye anaona sababu lukuki za kulifanikisha lile ambalo unataka kulifanya. Naye si mwingine bali ni VITABU.

Wako marafiki wengine ambao wana mitazamo hasi, wanaamini  katika kushindwa na pengine kuwa na sababu na visingizio vingi vya kutofanya au kuendelea na kile wanachokifanya.

Wanaopenda Kukata TAMAA kila wakati, Wasiotaka kujifunza kila siku, wasiotaka kukosolewa na mengine mengi.

HAWAKUFAI WATU WA AINA HII, na una kila sababu ya kuwaacha na kuchagua marafiki wengine wazuri wanaoweza kukusaidia, kukufundisha, kukuelekeza njia sahihi ya kufika kule ambako wewe unataka kufika.

Bila shaka Rafiki KITABU ndiye rafiki bora sana na ambaye kila mmoja wetu anapaswa kuomba Urafiki  naye na kasha kuambatana naye kwa kila hatua ambayo tunazipiga kila siku.

Na sio KITABU tu bali KITABU SAHIHI, huyu  atakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika, huyu anakuletea story za watu mbalimbali waliotangulia ambao walifanya mambo mbalimbali, wengine walishindwa na wengine walifanikiwa sana.

Rafiki huyu atakusimulia story ya wale ambao hawakuona sababu hata moja ya kukata tamaa licha ya changamoto mbalimbali ambazo walikabiliana nazo, mfano Kukosa PESA, KUKATALIWA, ULEMAVU na zinginezo nyingi ambazo wewe unazifahamu au kuzisikia.

Bila shaka kwa kusimulia story hizi za kweli zitakuhamaisha wewe na pengine  kukupa nguvu zaida  kusonga mbele bila ya kukata tamaa.

Na rafiki huyu anayo orodha ya watu wengi ambao waliwahi kufanya kile ambacho wewe unatamani kukifanya, kwa kupitia kuwafahamu watu hawa utajifunza njia ambazo wao walizitumia, changamoto na mafanikio makubwa sana ambayo waliyapata.

Na utajua ni wapi pa kuanzia safari yako, milima na mabonde na namna utakavyoweza kukabiliana nayo.

Lakini  rafiki huyu KITABU atakuunganisha na watu wengine wakubwa na wenye Hekima na Busara katika kufanya mambo mablimbali. Waflame, Wafanya biashara wakubwa, Bilionea na watu wenye sifa mbalimbali hapa duniani.

Anakufungulia dunia nzima na kuileta mahali ulipo, unapata nafasi ya kuyafahamu mambo mbalimbali kwa upana wake.

Bila shaka hautajuta kabisa kuwa naye maishani mwako.

This is my best friend ever to have on earth, because teaches me and direct me in the right way.

Huyu ndiye rafiki ambaye mimi rafiki yako nakuletea kwako hivi leo, tafadhali fanya urafiki naye, na kamwe hautajua kabisa kumfahamu.

 

MUHIMU; Ambatana nasi katika mtaa wetu ambako rafiki huyu ninayekusimulia habari zake kila siku anapatikana, na huku tunapiga naye story na hakika anatufundisha mambo mengi sana ambayo yanatufaa katika maisha yetu ya kila siku, na kutupatia UFAHAMU, MAARIFA NA UFAHAMU.

Mtaa huo unaitwa Street of Books (Mtaa wa Vitabu) huku tunayo mada moja tu ya KUJIFUNZA NA KUSOMA VITABU.

Karibu sana katika mtaa huu kwa sababu ni mtaa bora sana kuwahi kuwahi kuwepo.

Kujiunga na sisi tembelea mtandao wa Instagram kwa jina hili @streetofbooks_ na utakuwa miongoni wa wana mtaa huu.

Ahsanteni sana na Mungu akubariki sana kwa kujifunza name katika makala hii.  Usikose kutufuatilia katika ukurasa wetu wa Instagram wa @streetofbooks_ kila siku ili kujifunza zaidi na kupata hamasa ya kusoma vitabu na kupata maarifa yaliyomo humo.

 

Makala hii imeandikwa na;

Joshua Golyama

(Mwandishi, Mwalimu, Blogger na Mwazilishi wa Taasisi ya Elimu Kitaa Foundation).

Mawasiliano;  +255 764 257 495/.

Baruapepe; golyama.joshua98@gmail.com au elimukitaa2020@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...