Skip to main content

ANZA SASA, UMRI USIWE KIKWAZO CHA WEWE KUTOTIMIZA NDOTO ZAKO

 ANZA SASA KUFANYA, UMRI ISIWE KIKWAZO KWAKO.


Bila shaka unayo maono fulani (Unajiona ukiwa unafanya kitu baadaye ambacho ni kikubwa sana). Kwa namna fulani unatambua jambo fulani unaweza kulifanya kwa ufanisi mkubwa kabisa.


Na unajua kabisa, kwamba utakapofanya jambo lile utakuwa katika viwango fulani vikubwa sana.


Lakini, mbona huanzi? Nini kinakukwamisha usiendelee? 

Ni ujuzi, Maarifa, huelewi pa kuanzia? Au unasema ngoja nikue kidogo au nifikie hatua fulani?.


Tuko watu ambao tunasubiri hadi tufike viwango fulani vya Elimu ndipo tuanze kutumiza ndoto zetu.

Tuko watu tunaosubiri tufikie Umri fulani ili tuanze kutimiza ndoto zetu.


Lakini tunajichelewesha wenyewe, umri sio tatizo kabisa.

Kwani haujaona Watu wakiwa na Umri mdogo na wanafanya Makubwa?.


Je, Mastaa wengi katika tasnina mbalimbali duniani wana Miaka mingapi hadi muda huu na walianza wakiwa na Miaka mingapi?


Je, Mabilionea wa Dunia wana Miaka mingapi muda huu?.

Je unamfahamu Rev Victor Githu  kutoka Kenya  ambaye alianza  kuhubiri akiwa na Miaka Mitano (5) na sasa anafanya vizuri sana.


Je, Wewe una miaka mingapi hadi muda huu? Na bado unasema wacha nikue kue. 


Je, Haujasoma Biblia;  Wafalme walianza Kutawala wakiwa na Miaka mingapi? 

Ngoja Nikuonyeshe kidogo hapa.

Manase alianza Ufalme akiwa na Miaka 12 (2 Nyakati 33:1)

Yoashi alianza kutawala akiwa na Miaka 7.(2 Nyakati 24:1).

Yosia alianza akiwa na Miaka 12 ( 2 Nyakati 34:1)

Na wafalme wengi  waliotawala  Taifa la Israel walianza wakiwa na Miaka  20-25, Wakiwa bado wadogo kabisa.


Na iko mifano mingi sana na Ya watu ambao wameanza Kutumiza Malengo na ndoto  zao wakiwa wadogo kabisa (Vijana).


Nini kinachokuzuia wewe kutoanza.


Jiamini wewe mwenyewe (Believe on yourself that you can do great things according to the vision you have)


Unakumbuka Mungu alimwambia nini Yeremia wakati anajitetea kwamba Yeye ni mtoto mdogo.


Yeremia 1 (SUV)

¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯

⁷ Lakini Bwana akaniambia, _Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru._ 

⁸ _Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana._.


Hadi hapo sasa,  naona umeshaacha kujitetea ety kwa sababu ya Umri.


Hakuna sababu inayoweza kukuzuia wewe kutotimiza ndoto zako. Jiamini na anza kuchukua hatua sasa.


Usitake kuanzia pa kubwa, anza kidogo kidogo kwa Uaminifu mkubwa na Uvumilivu mkubwa na Kujitoa bila shaka utaushangaza ulimwengu  kwa kutimiza ndoto zako 


Kumbuka; Kutotimiza ndoto zako ni kuwanyima haki wale ambao wangefaidika na kutimizwa kwa ndoto zako.

Anza sasa, Umri ni namba kwa kuwa UPO UWEZO MKUBWA NA WA KIPEKEE ambao umewekwa ndani yako.


See You Shining And Enjoying The Cake!! 


Joshua Golyama 

+255 764 257 495

elimukitaa2020.blogspot.com

Elimu Kitaa Foundation

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...