Skip to main content

KUWA MAKINI SANA NA NAMNA UNAVYOTUMIA MUDA WAKO

KUWA MAKINI SANA NA NAMNA UNAVYOTUMIA MUDA WAKO

"Muda ni wa thamani sana kuliko fedha , unaweza kuzipata fedha kila siku Lakini muda hauwezi kuupata ukishaupoteza.
Hivyo, tunatakiwa muda vizuri ule tunaoupata na kwa umakini mkubwa zaidi.

Epuka kupoteza muda kwa kutofanya yale yasiyo na umuhimu kwako.
Maana wengi tunahangaika na mambo mengi sana ambayo hayana mchangi wowote katika maisha yetu.

Pale upatapo nafasi ya kufanya jambo, hakikisha unalikamilisha na kwa usahihi kabla ya kuanza kufanya jambo jingine.

Wekeza muda wako kwa kujifunza zaidi , wekeza zaidi ndani yako, ilishe akili yako maarifa mapya kila siku ili kuweza kuwa na mabadiliko makubwa hapo baadaye.

Wekeza ndani yako kwa kusoma vitabu, kusoma Makala na kuhudhuria semina mbalimbali
Jifunze kila siku na hii ni ni namna sahihi ya kutumia muda wako Vizuri.

Huwa napenda kusema kuwa, watu wengi tunalalamika na kukiri kwamba " muda mchache , na Mambo mengi,

Swali langu ni hili Je,  hayo Mengi uliyo nayo yana mchango wowote katika maisha yako??"

 MUHIMU;  Maana Halisi ya Kupoteza Muda (kutoka kwangu binafsi) ni kuhangaika na kufanya mambo mengi sana ambayo hayana mchango wowote katika maisha yetu(maisha ya Kusudi).

Kaa chini, tafakari na kisha yajue malengo yako unayoyafanyia kazi na  ujue yale mambo yatakayokufikisha huko(ukamilisho wa malengo yako) na hangaika na hayo tu.

See you Shining and enjoying the cake!

Joshua Golyama
golyamajoshua@gmail.com
Simu;0764257495/0622163323
Blogu;

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...