Skip to main content

KURASA 03; Kama unataka kufanikiwa , zingatia kitu hiki

Habari rafiki mpendwa, 

Karibu sana kama makala hii ya Kurasa za Mafanikio  ili tujifunze na kupata mafanikio makubwa 

Wakati tukiwa wadogo, wazazi walikuwa wanatukataza kucheza na kushirikiana na baadhi ya watoto/familia fulani, na endapo hutawasikiliza    unapata adhabu kubwa sana.
Na walitukataza pia kutokula  katika familia hizo.

Na zipo familia/watoto fulani ambao wazazi wanakuruhusu kwenda kucheza na kushirikiana nao na pengine wakakuruhusu kula chakula katika familia ile na hata kulala pale pale.

Na sababu kubwa ilikuwa  ni kuhakikisha  hatuharibiki katika tabia zetu .Na Katazo hilo lilikuwa linakuja baada ya Kutoridhishwa na tabia za watoto hao.

Jambo hili linaweza kutusaidia kujifunza machache kuhusu mchango wa wanaotuzunguka katika tabia zetu.
Ukiambatana na mwenye tabia ya  wizi, bila shaka utajifunza kuhusu wizi .
Ukiambatana na mwenye tabia ya Uongo, bila shaka nawe utakuwa na tabia hiyo hiyo.
Ukiambatana na msengenyaji bila shaka yapo machache utajifunza kutoka kwake.

Tunaposoma Maandiko Matakatifu , tukajifunza kitu kizuri sana kuhusu  wale wanotuzunguka.
Mithali 22:24 " Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi
Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi"

Usifanye urafiki na yule asiyependa kusoma kama wewe unataka kufaulu darasani usjie ukajifunza kuwa hivyo
Usifanye urafiki na muongo, kwa maana utajifunze tabia ya kuwa muongo
Usifanye urafiki na mtu asiyependa kuchukua hatua maana utajifunza kuwa na tabia hiyo.

Upo usemi unaosema "ukitembea na mwizi, nawe utakuwa mwizi"
Wale wanaokuzunguka wana mchangi mkubwa sana katika mafanikio yako, na mwenendo mzima wa maisha yako.

Kama unataka kufanikiwa katika maisha yako lazima uwe makini na aina ya watu  unaombatana nao.
Ni lazima uchague watu walio sahihi kutokana na sehemu ile au mafanikio unayotaka kuyafikia katika maisha yako.

Aslimia 85 (85%) ya furaha yako na mafanikio inatokana na Aina ya mahusiano uliyo nayo.
Kadiri una vyokuwa na mahusiano mazuri na imara ndivyo unavyoweza kufanikiwa sana.
Na aina ya mauhsiano uliyo nayo yanatabiri ni mafanikio ya kiwango kipi na aina gani utakayokuwa nayo.
Vile unakuwa na mahusiano/urafiki chanya katika maisha yako, ndivyo nawe unavyokuwa chanya zaidi

Hii ina maana kuwa ukiambatana na watu waliofanikiwa/ wenye kiu na mafanikio nawe una nafasi kubwa sana ya kufanikiwa na kuwa kama wao.

Pia asilimia 90(90%)  ya mafanikio yako , inategemea na wale wanakuzunguka(reference group)
Reference group(wanaokuzunguka) ni wale ambao unakuwa nao pamoja muda mwingi na baadhi ya vitu mnafanana katika kuvifanya.
Hivyo unatakiwa kuwa  makini sana na wale wanaokuzunguka wakoje?

Sisi binadamu tunafananishwa na Kinyonga, ambaye hubadilika na kufanana na mazingira alipo kwa wakati ule.
Ndivyo ilivyo hata kwetu, tunachukua mitazamo, tabia, thamani na hata imani kutoka kwa wale wanaotuzunguka.

Hivyo unapochagua aina gani ya mtu unataka kuambatana naye, ni lazima ujifunze kwanza ana sifa zipi na je,   zinazoweza kukusaidia wewe kufika sehemu sahihi /kule ulikokusudia.

Ambatana na wale walio na mitazamo chanya, wasiokata tamaa, wenye kiu na shauku ya kufanikiwa 
Kama ni maanafunzi ambatana na wanafunzi wale wanaopenda kusoma , na usiambatane au kufanya urafiki na yule asiyependa kusoma, na asiye na kiu ya kufaulu mitihani 

Kama unataka kuwa mtu aliyefanikiwa , huna budi kuambatana na wale wenye kiu na shauku ya kufanikiwa zaidi, na fanya urafiki nao.
Ambatana na wale mnaofanana vile unataka kufanya katika maisha yako.


Ondoka na uwe mbali sana na wale wenye mawazo hasi, mitazamo hasi na walalamikaji na wenye kulamumu kila wakati na sio watu wa kuchukua hatua.
 " Kama unataka kuruka juu kama Tai, ambatana na tai utaweza kuruka.

Ukitaja kufanikiwa ambatana na waliofanikiwa au wenye shauku ya kufanikiwa. Kuwa makini sana na aina ya watu unaombatana nao kila siku, kwa sababu wana mchango  mkubwa sana katika mafanikio yako.


_____________________________________
Makala hii imeandikwa na ; 
Joshua Golyama, ambaye ni Mwalimu, Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo, Mhamasishaji Wa Mafanikio na Mwandishi.

+255 764 257 495 / +255 622 163 323
Barua pepe; golyamajoshua@gmail.com
Blogu; elimukitaa2020.blogspot.com


Comments

  1. Amen,, asante ujumbe mzuri sanaa,, shukran kwa kutukumbusha watu tupasao kushirikiana na kuambatana nao ili kufikia mafanikio yetu 🙏🙏🙏

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante sana, Ubarikiwe sana nawe kujifunza haya,
      Endelea kutembelea tovuti hii kwa mafunzo mengi zaidi

      Delete
    2. Ubarikiwe sana, kaka karibu sana

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...