Skip to main content

KUTOKA VITABUNI 01_KILA KITU KINA MAANA KULINGANA NA MAANA YA MHUSIKA

 You give a meaning to every thing you see.

Nimekuwa nikisema kuwa, hakuna kitu kibaya au kizuri, ila mtazamo wako ndio unaweza fanya hivyo.

Namna ambavyo wewe unalitazama jambo fulani, ndivyo linavyokuwa na namna hiyo, na haitaweza kufanana na mwingine.

Mtu fulani ni mzuri au mbaya kulingana na namna ambavyo unavyomtazama.

Leo nakuambia kuwa, Kila kitu kinapewa tafsiri na wewe.

Hakiwi kizuri au kibaya, ila ni kwamba namna ambayo wewe umetoa tafsiri au maana hiyo.

Jambo laweza kutokea hapa na kushuhudiwa na watu wawili, kila mmoja akalipa maana yake.

Hivyo unavyosema jambo fulani ni zuri au baya ni kwa namna tu wewe uonavyo na si wote wanaona hivyo.

Usemavyo tu fulani anafaa au hafai, ni namna tu ambavyo wewe umemtafsiri na sio wote wamemtafsiri hivyo.

Tafsiri au maana ya jambo ulipalo wewe, kamwe halitafanana na mtu mwingine.

Ni wewe uonavyo hivyo, sio wote tunaona hivyo.

Wamuona mtu fulani ni mbaya, ni vile  wewe unaona hivyo na sio wote.

Usituaminishe au kutuambukiza tafsiri au maana ya kitu fulani uliyo nayo wewe.

Usituambize chuki uliyo nayo kwa mtu mwingine, kwa kuwa sivyo mwingine aonavyo.

Ndivyo maisha yalivyo, kila mmoja na maana yake.

You give meaning to everythiny you see

©Kiss That Frog.

Unaweza jifunza zaidi kwa kusoma.

1. Kitabu kifupi nilichoandika kwa kugusa maneno haya hapa chini RAFIKI BORA NI KITABU bila shaka utajifunza na kubarikiwa zaidi.


Makala hii imeandikwa na;

Joshua Golyama

(Mwandishi, Mwalimu, Blogger na Mwazilishi wa Taasisi ya Elimu Kitaa Foundation).

Mawasiliano;  +255 764 257 495/ +255 622 163 323.

Baruapepe;golyamajoshua@gmail.com auelimukitaa2020@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...