Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2022

#NAJIFUNZA_05: MAARIFA SAHIHI NA YA KUTOSHA KWA MAFANIKIO YAKO

 George Bernard Shaw aliwahi kusema maneno haya......"beware of false knowledge, it is more dangerous than ignorance" Kwamba "Kuwa makini sana na taarifa zisizo sahihi,  kwa sababu ni hatari zaidi kuliko ujinga" Taarifa ni kitu cha msingi sana, unapohitaji kufanya jambo fulani. Ukweli ni kuwa unahitajika kuwa na taarifa nyingi, kabla ya kufanya jambo. Lakini taarifa hizo lazima ziwe sahihi sana, kwa sababu zisipokuwa  sahihi zitakupelekea mahali pabaya. Ili ufanye vyema katika jambo fulani, unalazimika kuwa na taarifa nyingi na zilizo sahihi. Kuwa makini sana na vyanzo vya taarifa yako Fanyia tathmini kwanza, juu ya chanzo cha taarifa, Je, ni sahihi na zitakufaa. Kumbuka, Maamuzi yoyote yale yanategemea taarifa ulizo nazo. Kufeli au kufanikiwa kunategemea na taarifa ulizo nazo. Kiwango cha usahihi wa taarifa huamua aina ya matokeo ambao unakwenda kuyapata. ..Wito wangu ni kuwa, tuko katika karne ya TAARIFA, karne ambayo walio na taarifa sahihi ndio wanaofanikiwa. Na...

KUTOKA VITABUNI 01_KILA KITU KINA MAANA KULINGANA NA MAANA YA MHUSIKA

  You give a meaning to every thing you see. Nimekuwa nikisema kuwa, hakuna kitu kibaya au kizuri, ila mtazamo wako ndio unaweza fanya hivyo. Namna ambavyo wewe unalitazama jambo fulani, ndivyo linavyokuwa na namna hiyo, na haitaweza kufanana na mwingine. Mtu fulani ni mzuri au mbaya kulingana na namna ambavyo unavyomtazama. Leo nakuambia kuwa, Kila kitu kinapewa tafsiri na wewe. Hakiwi kizuri au kibaya, ila ni kwamba namna ambayo wewe umetoa tafsiri au maana hiyo. Jambo laweza kutokea hapa na kushuhudiwa na watu wawili, kila mmoja akalipa maana yake. Hivyo unavyosema jambo fulani ni zuri au baya ni kwa namna tu wewe uonavyo na si wote wanaona hivyo. Usemavyo tu fulani anafaa au hafai, ni namna tu ambavyo wewe umemtafsiri na sio wote wamemtafsiri hivyo. Tafsiri au maana ya jambo ulipalo wewe, kamwe halitafanana na mtu mwingine. Ni wewe uonavyo hivyo, sio wote tunaona hivyo. Wamuona mtu fulani ni mbaya, ni vile  wewe unaona hivyo na sio wote. Usituaminishe au kutuambukiza tafsi...