Skip to main content

#NAJIFUNZA_05: MAARIFA SAHIHI NA YA KUTOSHA KWA MAFANIKIO YAKO

 George Bernard Shaw aliwahi kusema maneno haya......"beware of false knowledge, it is more dangerous than ignorance"

Kwamba "Kuwa makini sana na taarifa zisizo sahihi,  kwa sababu ni hatari zaidi kuliko ujinga"

Taarifa ni kitu cha msingi sana, unapohitaji kufanya jambo fulani.

Ukweli ni kuwa unahitajika kuwa na taarifa nyingi, kabla ya kufanya jambo.

Lakini taarifa hizo lazima ziwe sahihi sana, kwa sababu zisipokuwa  sahihi zitakupelekea mahali pabaya.

Ili ufanye vyema katika jambo fulani, unalazimika kuwa na taarifa nyingi na zilizo sahihi.

Kuwa makini sana na vyanzo vya taarifa yako

Fanyia tathmini kwanza, juu ya chanzo cha taarifa, Je, ni sahihi na zitakufaa.

Kumbuka, Maamuzi yoyote yale yanategemea taarifa ulizo nazo.

Kufeli au kufanikiwa kunategemea na taarifa ulizo nazo.

Kiwango cha usahihi wa taarifa huamua aina ya matokeo ambao unakwenda kuyapata.

..Wito wangu ni kuwa, tuko katika karne ya TAARIFA, karne ambayo walio na taarifa sahihi ndio wanaofanikiwa.

Na kumbuka pia, Karne hii kuna mafuriko makubwa sana ya taarifa, kila mmoja anatoa taarifa zake anazozijua.

Hivyo, usipokuwa makini unaweza kupotezwa kabisa.

Hakikisha unatathmini usahihi wa taarifa kabla ya kuzifanyia maamuzi.

NB: Hii inafanya kazi maeneo yote ya Maisha, Hadi kwenye Ndoa kule, Usifanye maamuzi kama hauna taarifa sahihi.

Usisambaze taarifa ambayo hauna uhakika kama ni sahihi.

....... kumbuka Taarifa isiyo sahihi ni BOMU ambalo laweza kukulipua na kukuua kabisa.

Neno la Mungu kiwe ni chanzo cha kwanza kabisa cha taarifa zako zote, na vyanzo vingine vitafuata.

©Elimu Kitaa Foundation

Comments

Popular posts from this blog

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.

Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano; Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo. Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  si...

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...