ANZA SASA KUFANYA, UMRI ISIWE KIKWAZO KWAKO. Bila shaka unayo maono fulani (Unajiona ukiwa unafanya kitu baadaye ambacho ni kikubwa sana). Kwa namna fulani unatambua jambo fulani unaweza kulifanya kwa ufanisi mkubwa kabisa. Na unajua kabisa, kwamba utakapofanya jambo lile utakuwa katika viwango fulani vikubwa sana. Lakini, mbona huanzi? Nini kinakukwamisha usiendelee? Ni ujuzi, Maarifa, huelewi pa kuanzia? Au unasema ngoja nikue kidogo au nifikie hatua fulani?. Tuko watu ambao tunasubiri hadi tufike viwango fulani vya Elimu ndipo tuanze kutumiza ndoto zetu. Tuko watu tunaosubiri tufikie Umri fulani ili tuanze kutimiza ndoto zetu. Lakini tunajichelewesha wenyewe, umri sio tatizo kabisa. Kwani haujaona Watu wakiwa na Umri mdogo na wanafanya Makubwa?. Je, Mastaa wengi katika tasnina mbalimbali duniani wana Miaka mingapi hadi muda huu na walianza wakiwa na Miaka mingapi? Je, Mabilionea wa Dunia wana Miaka mingapi muda huu?. Je unamfahamu Rev Victor Githu kutoka Kenya ...
Hekima, Maarifa na Ufahamu Wekeza Saidia wengine