Skip to main content

KURASA 02; Kijue kile unachokipenda na ukifanye hicho.




Upo   usemi   unaojulikana   sana  katika mahusiano  ya  kimapenzi  "Ukipenda  Utakitunza" huu  ni  usemi  ambao  unatumika  sana  katika masuala  ya  mahusiano;

Ikiwa   na   maana hii, kwamba  kama  Kijana  anampenda   Binti  (kijana wa kike)  atatumia  kila namna   kuhakikisha  Binti  yule  anakuwa  katika hali nzuri , kwa   maana   ya  kumpendezesha  na  mambo  mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo.

Usemi huu,  una  ukweli  sana  katika  maisha  ya   kila  siku, na   pengine  huwa  tunautumia  msemo huu  bila  ya   kujua  kama zinaweza  kutusaidia katika   maisha   yetu   ya   Kila  siku .

Karibu    sana  katika  Kurasa  hii  ya  Asubuhi  ya  leo tuweze  kujifunza  juu  ya  kufanya  kile  unachokipenda   na   kuanza  kukifanyia  kazi .
Kufanya  kitu  usichokipenda   ni  hatari  sana 
Waliofanikiwa  hufanya  vile  vitu  wanavyovipenda. Huwezi  kufikia  mafanikio  makubwa  katika  Maisha  yako kama utashughulika  na  vile  usivyovipenda.

Tafuta kitu/jambo unalolipenda, kisha kifanye  hicho.
Penda  kazi  unayoifanya,  Penda  masomo  yako,  na  chochote  kile  unachokifanya 
Iko  nguvu  kubwa  sana  katika  kupenda.
 Ukipenda,  utajitoa   kikamilifu  kufanya 
Ukipenda , utakithamini na  kuitunza 
Ukipenda,  utahakikisha kinakuwa  bora  sana 
Na  utatumia  kila  unavyoweza   kuhakikisha  jambo  hilo  linafanikiwa 

Na  ukiipenda  kazi  unayoifanya,  hutakubali  kazi yako iharibike.
Na  kufanya  kazi  usiyopenda  ni  kupoteza  muda   na  haitakupa   ridhiko  la kutoka  ndani  na huwezi  kuona  Furaha  ya  kufanya  jambo  hilo/kazi  unayoifanya.
Kwa  wanafunzi  wa  Shuleni  na  Vyuoni 
Ili mwanafunzi aweze  kufaulu vizuri katika mitihani  ni  lazima  kwanza  alipende  somo  husika,  na  mwalimu  anayemfundisha .
 Asipolipenda  somo  hawezi  kuelewa na  akimchukia/kutokumpenda  mwalimu  hawezi  kumuelewa  mwalimu  wakati  anafundisha  na  kamwe  hawezi  kufaulu  hilo.

 Pale  unapokifanya  kazi  unayoipenda , hautaona ugumu  wowote  katika  kilifanya  kazi  hiyo. Pale wengine  wanapolalamika   na  ugumu wanaoupata,  kwako  inakuwa  rahisi sana kuifanya kwa sababu ni kazi unayoipenda kuifanya.

Hatua ya kuchukua;
Kijue   sasa   kile   unachokipenda   zaidi  kukifanya,  ambacho  hata  bila  kulipwa  unaweza  kukifanya. Kile ambacho hauko tayari kuona kinaharibika.  Kazi  ile  ambayo unatamani iwe bora zaidi.
Baada  ya  kukijua/kuijua , anza  kukifanyia  kazi,   fanya  kwa  bidii  na  jitoe  kikamilifu  kuifanya.
Tafuta  maarifa  ili  uweze  kuwa  bora  zaidi  katika  kazi  unayoifanya.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUANZA UPYA

  Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uz...

AGRICULTURE 101; KILIMO CHA TEMBELE

Habari   rafiki   mpendwa , Karibu   sana   katika   Makala   hii   Ya   Kilimo   na   Ufugaji Na   leo   tunakwenda   kuangalia   kuhusiana   na   Kilimo   Cha   Tembele. Mboga   nzuri   sana   na   inayopenda   na  kutumiwa   na    watu   wengi   sana   duniani Makala   hii   itakuwa   na   Sehemu/Vipengele   vifuatavyo; 1.Utangulizi 2.Aina za Tembele 3.Faida za Kiafya zitokanazo na Tembele 4.Namna Ya Kuandaaa Shamba 5.Kupanda 6 Kuvuna Karibu     sana    tujifunze   kuhusu    tembele. Kilimo cha tembele Kitaalamu    tembele   hujulikana   kama  ...

KARIBU KATIKA PROGRAM YA ELIMU KITAA(LEARNING SITE)

  Elimu Kitaa Foundation inakukakaribisha Katika Program ya Elimu Kitaa Habari ya kwako rafiki yangu. Bila shaka uko vizuri na unaendelea vyema na majukumu ya kila siku. Naitwa Joshua Golyama  mwanafunzi wa Shahada ya awali ya Sayansi ya Kilimo kwa Ujumla(Bsc.Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA                                         Mwanzilishi wa Program inayoitwa ELIMU KITAA. Leo ninapenda kukuletea maeneo mbalimbali ambayo unaweza yatembelea na tukajifunza pamoja na mimi. Maeneo hayo utapata nafasi ya kusoma makala ambazo ninaziandika kila siku na kuziweka humo, na tukajifunza kwa pamoja na kupata maarifa zaidi na zaidi. Kwanza kabisa nikupe utangulizi wa maana halisi ya Neno hili ELIMU KITAA. Elimu Kitaa ni program inayohusika na kuandika makala mbalimbali katika mitandao ya Kijamii na kuandaa semina mbalimbali zenye kutupa maarifa muhimu san...