MY MEMORIES _MY BRAIN REMEMBER THIS . Wakati nikiwa mdogo sana, nilijiona nikiwa mwalimu mkubwa sana na mwenye maisha fulani mazuri. Wakati mwingine nilikuwa na ndoto za kuwa daktari bingwa (Specialization). Ambapo kwa mara ya kwanza nilitamani sana kuwa Daktari aliyebobea kwenye masuala ya kutibu meno. Nikiwa naanza Kidato cha kwanza, wazo la ualimu liliendelea kuishi ndani yangu hadi kidato cha tatu, ambapo nilibadili wazo hilo na kuanza kufikiri kuwa Mhandishi wa Barabara (Civil Engineering) na nikaanza kuongeza juhudi kabisa katika Hesabu ili niweze kufanya vizuri katika hesabu na kupata nafasi ya kwenda kusomea Mchepuo wa PCM. Na ninachokumbuka ni kwamba katika mawazo yote hayo niliyokuwa na ndoto nilizokuwa nazo, nilipenda sana kuwaelekeza wengine pale ambapo hawaelewi na wakati mwingine kujipendekeza kuelekeza hata kama sijaombwa kufanya hivyo. Lakini baadaye kidogo (Mwishoni mwa Kidato cha nne), Nikawaza kuwa Daktari wa Masikio na wazo hili alilirudia mama yangu, baada ya...
Hekima, Maarifa na Ufahamu Wekeza Saidia wengine