Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2020

HEKIMA YA SIKU; Kila Jambo ulifanyalo lifanye kama wajibu na si kutegemea shukrani au kutambulika

Kila jambo unalolifanya, lifanye kama wajibu, na usifanye ukitegemea kutambuliwa, au kupewa shukrani. Watu wengi  wanapata shida sana  pale ambapo wanafanya mambo mengi, na hakuna anayeonekana kuwashukuru kwa yale wanayoyafanya. Unajitoa kwa nguvu zako kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa. Fuatilia mifano hii michache ili uweze kupata kile ninachokimaanisha hapa; Mfano  wa kwanza; Viongozi mbalimbali tulio nao, wanatumia muda wao mwingi na nguvu nyingi kuhakikisha wale wanaowaongoza wanafika pale wanapotakiwa kuwa. Na  hakuna hata mmoja anayetambua mchango wao na nguvu zao walizotumia kuwaongoza. Na pengine asiwepo hata mmoja wa kusema asante kwa yale wanayafanya. Mfano wa Pili ; kwenye mahusiano,unakuta boyfriend/girlfriend anafanya kila anachoweza ili kuboresha mahusiano yao, kumsaidia kwa kila hali/changamoto anayoipitia Lakini haoni mwenzie akimshukuru au kutambua kwa kile anakifanya. Mfano wa tatu; Kazini kwako, unafanya kila kitu vile inavyotaki...

KUWA MAKINI SANA NA NAMNA UNAVYOTUMIA MUDA WAKO

KUWA MAKINI SANA NA NAMNA UNAVYOTUMIA MUDA WAKO "Muda ni wa thamani sana kuliko fedha , unaweza kuzipata fedha kila siku Lakini muda hauwezi kuupata ukishaupoteza. Hivyo, tunatakiwa muda vizuri ule tunaoupata na kwa umakini mkubwa zaidi. Epuka kupoteza muda kwa kutofanya yale yasiyo na umuhimu kwako. Maana wengi tunahangaika na mambo mengi sana ambayo hayana mchangi wowote katika maisha yetu. Pale upatapo nafasi ya kufanya jambo, hakikisha unalikamilisha na kwa usahihi kabla ya kuanza kufanya jambo jingine. Wekeza muda wako kwa kujifunza zaidi , wekeza zaidi ndani yako, ilishe akili yako maarifa mapya kila siku ili kuweza kuwa na mabadiliko makubwa hapo baadaye. Wekeza ndani yako kwa kusoma vitabu, kusoma Makala na kuhudhuria semina mbalimbali Jifunze kila siku na hii ni ni namna sahihi ya kutumia muda wako Vizuri. Huwa napenda kusema kuwa, watu wengi tunalalamika na kukiri kwamba " muda mchache , na Mambo mengi, Swali langu ni hili Je,  hayo Mengi uliyo nayo...

KITABU CHA JUMA; My Philosphy For Successful Living -Falsafa Yangu Ya Maisha Ya Mafanikio.

KITABU CHA JUMA; My Philosphy For Successful Living -Falsafa Yangu Ya Maisha Ya Mafanikio. Habari ya kwako rafiki mpendwa, Natumai umekuwa na wiki ya baraka sana na bila shaka umepiga hatua kadhaa zenye kukusaidia katika safari hii tuliyonayo ya kulikamilisha kusudi la Mungu katika maisha yetu. Nikukaribishe katika makala hii ya kitabu cha Juma,  kutoka katika Kitabu Cha My Philosophy For Successful Living-Falasafa yangu ya Maisha Ya Mafanikio kilichoandikwa na Jim Rohn Jim Rohn ni Mjasiriamali wa Marekani, Mwandishi, na mhamasishaji Katika Juma hili tunakwenda kujifunza mambo machache na ya muhimu sana kutoka katika Kitabu hiki  cha My Philosophy For successful living Karibu sana tujifunze kwa pamoja mambo haya ambayo mwandishi anatufundisha katika kitabu hiki Kila mmoja wetu anatamani kuwa na maisha mazuri, hakuna hata mmoja anayetamani kuishi maisha ya shida. Lakini kutokana na ujinga wetu wa kutofahamu kanuni za Msingi za kuwa na maisha mazuri tunaishia k...